Maneno haya yana maana gani? “Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu HAMTOI ROHO KWA KIPIMO. (Yohana3:34)”

by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Tukianzia mistari ya juu anasema: 

Yohana 3:31 “Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.

32 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.

33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.

34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo

.35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia”. 

Kama tukichunguza hapo tunaona ni Kristo pekee ndiye anayeshuhudiwa katika biblia nzima kuwa “aliyaona na kuyasikia” mambo yote ya Mungu, Na hiyo ni kwasababu yeye alitoka huko, na asili yake ni huko, tofauti na wanadamu wengine wote, hivyo hata kile atakachokishuhudia duniani ni lazima kitakuwa ni Ukweli mtupu usiokuwa na chembe chembe yoyote ya mapungufu, Na ndio maana kila kilichotoka katika kinywa chake kilikuwa ni Neno la Mungu halisi kabisa.. Tofauti na manabii wake na watu wengine wote ambao wakati mwingine iliwapasa watafiti, tafiti wachunguze chunguze, 

1Petro 1:10 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

 Matendo 17:26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27 ili wamtafute Mungu, INGAWA NI KWA KUPAPASA-PAPASA, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu”. 

Vile vile mitume nao, japo walifunuliwa mambo yote na Roho mtakatifu lakini bado walikuwa hawana ufahamu wote wa mambo yote, 

1Wakoritho 13.9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika…….wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana”. 

Umeona, aliyefahamu mambo yote ni YESU KRISTO mwenyewe,ambaye hapo mwanzo alikuwapo kwa Mungu, yeye alikuwa ashuhudiwi kwanza na Roho ndipo aseme kama vile mitume walivyofanya, bali kilichokuwa kinatoka kwenye kinywa chake ni maneno ya ROHO mwenyewe akizungumza mbele za watu ndio maana aliwaambia mahali fulani, maneno yangu ni Roho tena ni uzima.

Yohana 6.63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”Hivyo mtu yeyote akiyasikia maneno ya Kristo, na kuyashika, ni Roho wa Mungu mwenyewe ndio anayejaa ndani yake..

Na ndio maana Yohana akamshuhudui, kuwa hamtoi Roho kwa kipimo. Leo hii ukisikiliza maneno ya watumishi wote wa Kristo, utapata kipimo cha Roho wa Mungu, kwasababu maneno yanayotoka katika vinywa vyao hajakamilika yote, lakini ukisikiliza maneno ya Kristo, utapata kiwango kamili cha Roho wake, kwasababu ni Neno lililotakasika lisilo la chembe ya uchafu, lisilo na kipimo …Na maneno ya Kristo ndio BIBLIA TAKATIFU,..ukiisioma hiyo, na kuiishi hiyo utapokea kiwango kamili cha Roho wake, bila kipimo…Kwasababu maneno yake ni ROHO. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?

JE MUNGU ANAMJARIBU MTU?


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/maneno-haya-yana-maana-gani-kwa-kuwa-yeye-aliyetumwa-na-mungu-huyanena-maneno-ya-mungu-kwa-sababu-hamtoi-roho-kwa-kipimo-yohana334/