Mtume Paulo alioa?

by Admin | 4 October 2019 08:46 pm10

Mtume Paulo, hapo kwanza alikuwa akiitwa SAULI, Alikuja kuitwa Paulo baada ya kukutana na Bwana Yesu, na kubadilishwa….Alizaliwa mahali panapoitwa Tarso, huko Kilikia,…Kwasasa ni eneo la nchi ya UTURUKI.

Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge”.

Kwa asili Paulo alikuwa ni Myahudi (yaani Muisraeli) alikuwa ni wa kabila la Benyamini na alikuwa ni Farisayo.

(Wafilipi 3.5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,)

Mtume Paulo hakuoa mke, Alijizuia kuoa ili aihubiri Injili pasipo kuvutwa na mambo mawili, yaani mambo ya kumpendezesha mke na kumpendezesha Mungu..

1Wakorintho 7 :32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”.

kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji na Eliya Nabii hao pia hawakuoa. Na hivyo kuwafanya Injili yao kuwa na matunda mengi kuliko wengine wote.

Biblia inasema hakuna Nabii aliyetokea aliye Mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, kadhalika Eliya ni nabii pekee ambaye hakuonja mauti..Na Mtume Paulo ni Mtume pekee ambaye alifanya kazi kuliko wote waliomtangulia.


Mada Nyinginezo:

YOHANA MBATIZAJI NI NANI?

YESU NI NANI?

SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/04/mtume-paulo-alioa/