Mungu hawezi kukusahau

by Admin | 5 October 2019 08:46 pm10

Kama unamcha Mungu kweli, na unakwenda katika njia zake, yeye ni mwaminifu hawezi kukusahau. Kabla maisha yako hayajaisha hapa duniani, atakuridhisha, atakufikisha mahali ambapo ni zaidi hata ya ulivyokuwa unafikiri.

Kama hakumsahau Yusufu, ambaye aliuzwa Kama Mtumwa Taifa la mbali kabisa, hawezi kukusahau wewe kama unakwenda katika njia zake.

Kama hakumsahau Musa ambaye aliacha hazina zote za Misri  na kwenda majangwani, hawezi kukusahau wewe uliyeacha kila kitu na kumfuata  Mungu..

Waebrania 11:26 “akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana”

Kama hakumsahau Hana aliyekuwa Tasa na kumpatia watoto wengi..Hawezi kukusahau wewe unayemcha leo, hajabadilika ni yeye yule vizazi na vizazi,

Isaya 49:14 “Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.

15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima”.

Mche tu yeye! Jitenge na uovu, kuwa mtumishi wake..Utauona wokovu wake, hatakusahau kamwe! hawezi kusema uongo. 

Isaya 44:21 “Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi”

Kinachowakosesha wengi ni dhambi katika maisha ya watu,vitu kama uasherati, usengenyaji, wizi, ulaji rushwa, utukanaji, ibada za sanamu, wivu, biashara haramu, uvaaji mbaya, kutokusamehe n.k hivyo ndivyo vitu vinavyoharibu mpango wa Mungu juu ya maisha yetu…Lakini mtu akijitenga na hivyo Kamwe Mungu hawezi kumsahau, haijalishi itapita miaka mingapi lakini atakuja kuuona utukufu wa Mungu maishani mwake.

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MNGOJEE BWANA

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?

“HERI WALIO MASKINI WA ROHO MAANA UFALME WA MBINGUNI NI WAO” JE HATUNA RUHUSA YA KUWA MATAJIRI KATIKA ROHO?


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/05/mungu-hawezi-kukusahau/