Je Kutoa Mimba ni dhambi?

by Admin | 20 December 2019 08:46 am12

Je Utoaji mimba/ kutoa mimba ni dhambi?..Je kama mtoto aliye tumboni anahatarisha uhai wa mama na madakatari wakamwambia anapaswa atoe hiyo mimba ili aishi vinginevyo atakufa..je endapo akiitoa ili kunusuru uhai wake kwa sababu za kiafya atakuwa amefanya dhambi ni muuaji?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu maana ya utoaji mimba..Utoaji mimba ni kitendo cha mzazi wa kike..kuondoa kiumbe ambacho tayari kimeshaanza kuishi katika tumbo lake..Hicho kinaweza kuwa katika wiki ya kwanza au katika mwezi wa mwisho wa 9. Hatua yoyote inayohusisha kukiondoa hicho kiumbe tumboni kwa mwanamke katika kipindi hicho cha muda  ni kitendo cha UTOAJI MIMBA.

Utoaji mimba umegawanyika katika sehemu mbili..1) Utoaji mimba kwa sababu za kiafya 2) Utoaji kwa sababu nyingine zisizo za kiafya.

Tukianza na sababu za kiafya

Hii inahusisha pale mama mjamzito..labda kaugua ghafla na ile mimba ndani ya tumbo lake ikaharibika au mtoto akafa tumboni…Ili kuokoa maisha ya mama analazimika kwenda kuiondoa hiyo mimba hospitalini..Katika hali kama hiyo mama huyo hafanyi dhambi kwasababu tayari mtoto kashakufa..hivyo anapaswa atolewe huko aliko na kuzikwa.

Pia Inaweza kutokea mimba ya mama mjamzito ikatoka yenyewe kabla ya wakati wake…Hali kama hiyo pia hakuna dhambi iliyotendeka..Ingawa sio kawaida mimba kutoka yenyewe…

Lakini pia inaweza kutokea Mama mjamzito kapata tatizo au ugonjwa ambao utamlazimisha aondoe ile mimba iliyopo tumboni mwake ili kunusuru uhai wake. Na asipofanya hivyo kuna hatari ya kufa. Katika hali kama hiyo ambayo imethibitishwa..endapo mimba hiyo akiitoa hafanyi dhambi. Kwasababu amefanya hivyo  ili kunusuru uhai wake…na asipofanya yeye pamoja na hicho kiumbe tumboni watakufa.

Lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa..Hata katika hali hiyo ambayo madaktari wamesema kwamba ni ngumu kunusuru uhai  wa mama akiwa na kiumbe tumboni..YESU KRISTO wa Nazareti hashindwi jambo..Mimba inaweza isitolewe na mwanamke huyo akazaa vizuri kabisa bila kufa wala kupata tatizo lolote..wanadamu wanashindwa mambo lakini Yesu Kristo hana rekodi ya kushindwa…Na wapo wanawake wengi wametendewa na Yesu miujiza kama hiyo…wamepewa ripoti na madaktari kwamba aidha waiondoe mimba waishi au waendelee kukaa na hiyo mimba wafe…lakini Bwana amewapigania na wameshinda vitisho vya vifo na wamejifungua salama kabisa bila tatizo lolote…Na waliotendewa hivyo na Yesu wapo wengi sana.

Lakini hiyo inahitaji imani thabiti isiyo na mashaka kwa Yesu Kristo…Lakini kama mtu ataingiwa na mashaka basi ni heri akaenda kuiondoa hospitalini…Kwasababu biblia imesema mtu asiye na imani asitegemee kupokea kitu kutoka kwa Mungu…

Yakobo 1.6 “… Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”

Sababu za PILI za kutoa mimba ni sababu zisizo za kiafya 

Sababu hizi zinahusisha…Pale mwanamke anapopata mimba na wakati hana mpango wa kuwa na mtoto kwa wakati huo…Mwanamke wa namna hiyo akiitoa mimba ambayo tayari kashaipata anafanya dhambi..ni Muuaji.

Mwanamke ambaye amepata mimba kwa kubakwa au kwa mtu asiyempenda na akaenda kuitoa anafanya dhambi tayari, ni muuaji.

Mwanamke ambaye kapata mimba na kalazimishwa na mtu aliyempa mimba kwamba aitoe na yeye akaitoa anafanya dhambi huyo ni muuaji kabisa.

Mwanamke ambaye kapata ujauzito na Baba aliyehusika na ujauzito huo kaikataa hiyo mimba na mwanamke akaenda kuitoa hiyo mimba anafanya dhambi  ni muuaji.

Mwanamke anayetoa mimba kwasababu ya umasikini au hali ngumu ya kimaisha kwa kuhofia malezi ya mtoto yatakuwaje anafanya dhambi ni muuaji.

Na sababu nyingine zote zilizosalia zisizo za kiafya..Ni dhambi kutoa mimba kwa kutumia hizo sababu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001812. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KUOTA UNA MIMBA.

Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?

KIELELEZO CHA MWANAMKE KATIKA NYUMBA.

Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/12/20/je-kutoa-mimba-ni-dhambi/