by Admin | 29 February 2020 08:46 pm02
2Wakorintho 5.17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”.
Kuwa kiumbe mpya sio kuwa “mtu mpya”…Mtu ni yule yule isipokuwa tabia zinabadilishwa….Mtu wa tabia za asili anania mambo ya ulimwengu huu…Furaha yake ni kula na kunywa na anasa kama mnyama tu. Mnyama kamwe hawezi kufikiri kwamba akifa ataenda wapi, na wala hajali chochote isipokuwa watoto wake tu…
Kikubwa katika maisha ya wanyama wanachokijua ni kula, kunywa, kuzaliana, kulea watoto wao na kujiburudisha katika mazingira tofauti tofauti. yanayopatikana katika mazingira ya ulimwengu huu basii…Hali kadhalika hali yake mtu ambaya hajazaliwa mara ya pili..vitu vya pekee vinavyoutawala ufahamu wake ni kuwa na maisha bora katika kiulimwengu huu, aoe/aolewe…awe na nyumba nzuri, awe na mali na maisha bora…na baada ya hapo afe.
Hakuna chochote kinachomhimiza afikiri kuwa kuna maisha baada ya hapa. Fungu lake lipo katika ulimwengu huu.
Lakini mtu aliyezaliwa mara ya pili..biblia inasema anakuwa amevuka kutoka mautini kuingia uzimani, na anakuwa amefanyika kiumbe kipya…akili yake inakuwa imebadilishwa na kuwa akili ya kimbinguni..mawazo yake yanaelekea mbinguni tu…
Vitu vya ulimwengu huu avipate au asivipate hiyo inakuwa haimsumbui sana kwasababu anajua anao utithi wa mbingu zilizo tajiri kuliko mamlaka zote na falme zote duniani.
Je ya kale yamepita kwako? je umefanyika kiumbe kipya?
Kama bado unasubiri nini usiingie ndani ya Yesu leo?..Mkabidhi Yesu maisha yako uokolewe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/29/ya-kale-yamepita-tazama-yamekuwa-mapya/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.