Tofauti kati ya kuungama na kutubu ni ipi?

by Admin | 27 May 2020 08:46 am05

Kuungama kunakwenda sambamba na kutubu.

Kuungama ni kitendo cha kukiri, au kukubali makosa yako kuwa wewe ni mwenye dhambi au ulikosa na hivyo unahitaji kusamehewa.

Mathayo 3:5 “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;
6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao”.

 

Matendo 19:17 “Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao”.

 

1Yohana 1:8 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

Lakini kutubu ni kitendo chenyewe cha kujutia  yale uliyoyaungama tayari (yaani makosa yako)..Ili usamehewe. Na hii inaambatana na kukusidia kuyaacha kivitendo yale uliyokuwa unayafanya kwa kuomba msamaha .

Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.

 

Mathayo 21:28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu.

29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.

30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.

31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.

32 Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.”

Na ndio maana mtu hawezi kusema nimetubu kama hajaungama dhambi zake, Yaani hajakubali kuwa amekosa mbele za Mungu, kwamba yeye ni mwenye dhambi na hivyo anahitaji rehema.

Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema”.

Hivyo kutubu kunaambatana na kuungama, kama ukienda mbele za Mungu halafu huoni kosa lako nini, basi hapo hakuna toba yoyote.

Ubarikiwe.

 

Mada Nyinginezo:

Kwanini Bwana alirejea Tiro na Sidoni kwa mfano wa Sodoma?

Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?

 

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/05/27/tofauti-kati-ya-kuungama-na-kutubu-ni-ipi/