by Admin | 14 January 2021 08:46 pm01
Buruji ni aina ya mnara ambao ulijengwa zamani mahususi kwa ajili ya kuvamia kambi za maadui zilizojengwa kwa kuta ndefu.
Kwa namna ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuvamia ngome za namna hiyo..kwani askari walikaa juu ya kuta hizo ndefu wenye mishale ya moto na mawe mazito..kwahiyo kama nyinyi mtakwenda kushindana nao kwa njia za kawaida kwa pale chini. Kitakachokuwa kinaendelea ni kifo tu.
Hivyo iliwabidi wabuni njia nyingine za kuwashambulia maadui waliojizungushia boma juu ya kuta..ndipo hapo sasa yakagunduliwa haya maburuji..ambayo kwa chini yalikuwa na matairi manne..na urefu wake ulilingana na zile kuta za maadui zao au zaidi kidogo..hivyo askari walikuwa wanapanda mpaka juu kabisa mwa maburuji hayo…mahali ambapo watakuwa usawa mmoja na wale maadui zao..kisha wanaanza kuwashambulia..huku wanazidi kuusogelea ukuta wa mji kidogo kidogo.
Na wakishafanikiwa kufika kwenye ukuta wanashusha ngazi zao..kisha wanashuka kutokea huko huko juu na kuingia katika mji na kuanza kuwashambulia.
Tazama picha juu uone jinsi zilivyotengenezwa
Kwa kuwa buruji hizo zilikuwa zinajengwa kwa mbao..sasa ili kuzuia moto kutupwa kuziteketeza..walizizungushia chuma au ngozi za wanyama kiasi kwamba mishale ya moto hata ikitupwa haikuweza kuleta madhara.
Isaya 23:13
[13]Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; WAMESIMAMISHA BURUJI ZAO ZA VITA, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Pia kibiblia minara yote ya maficho iliyokuwa ndani ya ngome iliitwa kwa jina hili
Vifungu hivi vinaelezea neno hilo.
Waamuzi 9:46
[46]Kisha watu wote waliokaa katika ile buruji ya Shekemu waliposikia habari hiyo wakaingia ndani ya ngome ya nyumba ya El-berithi.
2 Mambo ya Nyakati 26:15
[15]Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya
na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
Soma pia Waamuzi 9:47,49 Yeremia 31:38, Sefania3:6 Wimbo 8:9 Nehemia 3:8
Halikadhalika pia kiroho zipo kuta nzito adui yetu ibilisi ameziweka mbele yetu.. lakini Tukimtumainia Bwana yeye mwenyewe ndio atakuwa buruji letu. Hatuhitaji nguvu za mwilini kupambana naye..bali zile za Rohoni..Wana wa Israeli walimwamini Mungu na wakafuata maagizo yake kwa ukamilifu..na walipokutana na zile kuta za Yeriko, sote tunafahamu ni nini kilitokea..ni kwamba zilizama chini zote..pakawa tambarare kama vile hakujawahi kuwa na kuta au ngome..
Halikadhalika na sisi tunahitaji kumwamini Mungu na kuishi sawasawa na njia zake. Na hayo mengine ya vita vya ibilisi yeye atayashughulikia mwenyewe kirahisi kabisa.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka?Je umepata uhakika kama ukifa leo utakwenda wapi?..una habari kuwa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba zile dalili zote za kuja kwa Yesu zimeshatimia tunachongojea sasa ni Unyakuo tu?
Unangojea nini? Tubu mrudie muumba wako katika hizi dakika za lala salama.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/01/14/neno-buruji-lina-maana-gani-katika-biblia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.