WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

by Admin | 29 January 2021 08:46 am01

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki…..

48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.

Kumuombea anayekuudhi sio kitu kirahisi hata kidogo, huo ndio ukweli..afadhali ungeambiwa achana naye tu yapite, lakini unaagizwa  umuombee, si jambo jepesi, Lakini hivyo ndivyo vipimo vya ukamilifu wa mtu kwa Mungu. Hakuna njia ya mkato.

Pale unapoona jirani yako anakuzungumzia vibaya, mpaka anakuharibia  pengine siku yako, badala umchukie na kumwekea vinyongo, au umzungumze na wewe vibaya , unaambiwa na Yesu umuombee.. Ukishindwa kufanya hivyo, basi wewe bado hujawa na tabia kama za Mungu ndani yako, bado hujawa mkamilifu kulingana na maandiko.

Bwana Yesu alitoa, mfano hai akasema, hata Mungu mwenyewe, huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua yake waovu na wema..Kiasi kwamba mchawi anatoka kuwaloga watu usiku, na kuwasababishia matatizo, lakini asubuhi anaamka na mvua kwenye shamba lake, na linastawi vizuri yake , mpaka anavuna, na kuuza, na kupata chakula kwa ajili yake na watoto wake na cha akiba.

Jambazi, anatoka kuiba usiku na kuharibu, na akiamka asubuhi anakutana na jua kama wewe unavyoliona, sio kwamba Mungu anapendezwa na tabia zake, la, lakini anaonyesha rehema zake kwao pengine siku moja watatubu, na kuacha njia zao.

Na sisi pia kuna wakati tulishawahi kuwa waovu mbele za Mungu, kiasi kwamba ilikuwa ni haki ya Mungu atulipizie kisasi tuondoke chini ya jua, lakini mara nyingi tumeona hakufanya chochote, mpaka sasa tumetubu tumeokolewa, na tunamtumikia. Laiti kama asingekuwa mvumilivu kwetu, leo hii tungekuwa kwenye moto wa jehanumu.

Huo ndio ukamilifu wa Mungu, na yeye pia akatupa agizo hilo hilo kwamba tuwaombee wale wanaotuudhi, wale ambao tunawaona ni maadui zetu haswa haswa, tuwaombee, tusijifanye sisi ni washupavu sana, tunajua kupambana, tunajua kusimamia haki zetu, tukadhani kuwa mawazo ya Mungu ni kama ya kwetu, badala ya kuwaombea mema, tukaanza kuwaombea vifo, kuwaombea njaa, kuwaombea wasifanikiwe..n.k.

Mungu atahuzunishwa na sisi, na kutuona kama ni wachanga ya njia zake.

Kumbuka hatujaitwa kuwaiga wanadamu, bali tumeitwa kumuiga Mungu. Kama vile Yesu alivyosema,…

Yohana 5:19 “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile”.

Haijalishi wanadamu wote watasema, wapige maadui zako. Lakini maneno ya Yesu ni tuwaombee. Hata kama yataonekana ni maombi magumu kwetu, lakini kwa Mungu ni manukato. Tujizoeshe kuwa watu na namna hiyo kila siku. Ndipo tutakapoona Mungu akituzidishia na sisi rehema zake kila siku.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/01/29/waombeeni-wanaowaudhi/