Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?

by Admin | 12 May 2022 08:46 pm05

Swali: Je Ni sahihi  kimaandiko kwa mwimbaji wa nyimbo za injili kufanya collaboration na wasanii wa kidunia?..


Kabla ya kujibu swali hili, hebu tujiulize kwanza swali lifuatalo!. Je ni sahihi Mchungaji kumwalika mtu wa kidunia ambaye hajaokoka kabisa aje kuhubiri madhabahuni?. Kama jibu ni Ndio!, basi pia ni sahihi Mwimbaji wa nyimbo ya Injili kushirikiana na msanii wa kidunia katika kuimba, lakini kama jibu ni hapana!! basi pia si sahihi mwimbaji wa nyimbo za injili kushirikiana na mwimbaji wa nyimbo za kidunia kumwimbia Mungu.

Jambo moja lisilofahamika na wengi, hususani waimbaji wa nyimbo za Injili, ni kwamba hawajui kuwa Huduma ya kumwimbia Mungu, ni huduma kama ya Uchungaji tu!..Unaposimama kumwimbia Mungu, ni sawasawa na umesimama madhahabuni unahubiri, na unaonya na unawajenga watu kiroho, sawasawa na uchungaji tu, au uinjilisti….

Sasa Unaposhirikiana na mtu ambaye hajaokoka utakuwa unaiharibu kazi ya Mungu, badala ya kuijenga, umempandisha shetani madhabahuni ahubiri..kwasababu yule mtu ambaye hajaokoka anazo roho ndani yake, ambazo ni za mashetani…maisha yake yanaongozwa na shetani, aidha kwa kujua au kwa kutokujua..kama ni hivyo atawezaje kusimama kuwahubiria wengine waokoke, wakati yeye mwenyewe hajaokoka, atawashaurije wengine waache ulevi wakati yeye mwenyewe ni mlevi na mzinzi, atawaambiaje watu wawe wasafi mwilini wakati yeye mwenye mwili mzima umejaa tattoo?.

Umeona? Tunaweza kushirikiana na watu ambao hawajaokoka katika kufanya mambo mengine ya kimaisha kama kazi (ukiwa ofisini au shuleni, utashirikiana na watu ambao hawajaamini, haina madhara), au unaweza kuishi nao, au kula nao… lakini SI KUFANYA NAO KAZI ZA MADHABAHUNI!!!.

Bwana Yesu alikuwa anakula na watoza Ushuru, na makahaba na wenye dhambi wote… lakini hakuwahi kuwatuma Pamoja na wakina Petro wakahubiri Injili!!.. Hakuna mahali Bwana Yesu kamtupa Adrea na Farisayo mmoja au kahaba wakafanye collaboration katika kuhubiri Injili!.. Kwasababu hilo kundi bado lilikuwa linahitaji kwanza kuhubiriwa liokoke na si kwenda kufanya huduma!.

Kwahiyo na sisi kama Watumishi tulioitwa katika kuutangaza ufalme wa Mungu kwa njia ya nyimbo na nyinginezo.. na kama tunataka kushirikiana Pamoja na watu wengine ambao kwasasa ni wa kidunia, (bado hawajaokoka)..Sharti kwanza TUWABADILISHE WAOKOKE!!!, watubu dhambi zao na kubadilisha Maisha yao, na baada ya kuokoka na kupata wokovu kamili, wakae kwenye madarasa ya kumjua Mungu kwa kitambo Fulani, na wakishafikia kiwango Fulani cha ufahamu wa kumjua Mungu, ndipo tushiriki nao katika kufanya huduma ya kumwimbia Mungu au uinjilisti, Ili kazi ya Mungu isiharibike wala kutukanwa!!.

Kwahiyo kwa hitimisho, ni kwamba sio sahihi kushiriki Pamoja na wasio amini kutangaza Habari za ufalme wa mbinguni..

Bwana atubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je ni sahihi kusikiliza miziki ya kidunia?.

USIWE ADUI WA BWANA

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?

Zaburi maana yake nini, katika Biblia?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/05/12/je-tunaruhusiwa-kushirikiana-na-wasanii-wa-kidunia-katika-kumwimbia-mungu/