Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala Mwangalie sana

by Admin | 13 January 2023 08:46 am01

SWALI: Mstari huu unamaana gani?

Mithali 23:1-3

[1]Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.

[2]Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.

[3]Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.


JIBU: Sulemani akiwa kama mfalme alielewa sana tabia za wafalme zilivyo na hivyo kwa uzoefu wake hapa anatoa mapendekezo yake kwa mtu yeyote ambaye ataitwa na mfalme au mtu yeyote mkuu kula chakula pamoja nao.

Anasema chukua tahadhari “Mwangalie sana”..uwe na kiasi na hizo zawadi zake akupazo, hapo ametumia lugha ya vyakula, lakini yaweza kuwa uongozi, fursa, pesa, n.k..anasema uwe na kiasi, kwasababu nyingi za hizo huwa ni za hila.

Kwasababu mfalme hawezi kumwalika mtu, kama haoni kuna faida fulani anaweza kuipata kwake, ingekuwa ni hivyo angekuwa anamwalika kila mtu tu, ikulu na kushiriki naye.

Mfano wa wazi tunauona, kwa malkia Esta alipomwalika Hamani, kama Hamani angelielewa andiko hili, angetafakari mara mbili mbili ni kwanini apewe tu yeye kipaumbele cha juu zaidi ya wengine..Lakini alikuwa anacheka na kufurahia tu mialiko, na matokeo yake yakawa ni kujipeleka mwenyewe kitanzini.

Ni kawaida ya shetani akishaona una hatari ya kuupindua ufalme wake, haji kwa hasira au kiboko, atakuja kwa anasa, alifanya hivyo kwa Bwana Yesu, na kumwambia “hivi vyote nitakupa, endapo utaanguka na kunisujudia”..Bwana akamkemea, na kumfukuza, wakati mwingine mfalme Belshaza alimwita Danieli, amtabirie vizuri juu ya ufalme wake akamuahidi atakuwa mtu wa tatu kwenye ufalme wake, Danieli hakupumbazika na kukaa pamoja naye katika utawala wake wa dhambi, kinyume chake akakataa akatabiri na kuondoka zake..Lakini usiku huo huo kumbe ndio ulikuwa mwisho wa mfalme Belshaza, akavamiwa na wamedi, na kuuawa, sasa kama Danieli angekutwa pale anafanya anasa nao naye pia habari yake ingeishia pale.

Watumishi wengi wa Mungu wakubwa, wamepoozwa moto wao wa injili au utumishi wao kwa ujumla na watu wakuu au wa mamlaka, kwa kukosa kwao kiasi. 

Hivyo mstari huu unatupa tahadhari, katika ngazi yoyote ile,  iwe ni ngazi ya chini, katika kampuni,au shirika,  au katika serikali, tualikwapo, tuwe makini, kuchunguza ni mashauri gani yapo nyuma yake.

Bwana akubariki.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU

NUHU WA SASA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/01/13/utakapoketi-kwa-chakula-pamoja-na-mtawala-mwangalie-sana/