Fahamu maana ya Warumi 14:7 hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake.

by Admin | 18 January 2024 08:46 am01

SWALI: Warumi 14:7 Inamaana gani?

“Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake”. 

JIBU: Ni andiko linalotuonyesha uweza wa Mungu ulivyo wa kutawala/ kuendesha vitu vyote. Kwamba mwenye maamuzi yote yahusuyo maisha ya mwanadamu ni Mungu, Wala sio nafsi ya mtu kama atakavyo yeye mwenyewe.

ikiwa na maana kuishi kwako unalitimiza kusudi fulani la Mungu,(haijalishi wewe ni mwema au mtenda maovu) vilevile kufa kwako ni matokeo ya kusudi Fulani la Mungu.

Vifungu vinavyofuata vinazidi kuelezea vizuri zaidi…Anasema;

Warumi 14;8 Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu MALI YA BWANA. 

Umeona?  Wanadamu wote ni Mali ya Bwana, Hakuna mtu aliyejiumba mwenyewe..akawa na maamuzi yake yanayojitegemea yasiyopitishwa kwanza na Mungu.. mtu hawezi kusema kesho nitajitoa uhai wangu na kuurudisha, au kesho nitafanya hiki au kile, bila Mungu kulijua au kuliruhusu, au kulipanga ,. Au aseme baadaye nitaliamuru jua lisichomoze kwa matakwa yangu, Hilo jambo haliwezekani.

Sisi wote hatuishi Kwa nafsi zetu(mapenzi yetu ) wenyewe, Bali Kila jambo kama sio limeagizwa na Mungu, basi Mungu ameliruhusu.. Hata vifo vyetu vivyo hivyo. Na vitu vyote tuvifanyavyo. Kwasababu sote tunamilikiwa na Mungu.

Ndio maana ya hilo neno “hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. ”

Bwana akubariki

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Bwana Yesu alikuwa kabila gani?

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)

Anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona anamaana gani?

NJIA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/01/18/warumi-147-hakuna-mtu-miongoni-mwetu-aishiye-kwa-nafsi-yake/