by Admin | 25 March 2024 08:46 am03
Je! wakristo tunalaumiwa?
JIBU: Ni mashtaka au maneno Fulani yanayotolewa dhidi yako, yanayolenga kutoridhishwa na mwenendo, au maneno au tabia yako.
Tunaweza tukawa watoto wa Mungu, na bado siku ile ya mwisho tukalaumiwa na Mungu. Utauliza ni kwa namna gani?
Ni kweli deni letu la mashtaka limeondolewa pale msalabani kwa Kifo cha Yesu Kristo. Na kwamba mtu anapomwamini tu Yesu Kristo haukumiwi, bali anaingia uzimani. Tafsiri yake ni kuwa hana lawama la hukumu ya jehanamu (Wakolosai 1:21-22)
Lakini, kumbuka wewe “unahesabiwa” kuwa mwenye haki. Lakini kiuhalisia “huna haki ndani yako”. Yaani kwa asili wewe huna kitu chochote kizuri ndani yako mbele za Mungu, na kimsingi huo sio mpango Mungu aliokusudia kwa mwamini. Mungu anataka amwokoe mtu wake, na wakati huo huo awe mkamilifu kama yeye.
Ndio hapo hatupaswi kuichukulia NEEMA ya Mungu kama fursa ya sisi kupumzika katika dhambi, au kupuuzia matendo ya haki. Au kutokuonyesha bidii yoyote ya Kufanana na Kristo.
Maandiko yanasema watu wengi wataonekana kuwa na lawama, mbele za Kristo, kwa kushindwa tu kurekebisha baadha ya mienendo yao, walipokuwa hapa duniani.
Kwa mfano maandiko haya yanaeleza baadhi ya mienendo, hiyo; moja wapo ni kukaa katika Mashindano, au manung’uniko ndani ya wokovu hupelekea utumishi wako,kulaumiwa .
Wafilipi 2:14 “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu”
Vilevile kutofikia upendo na Utakatifu, ni zao la lawama.
1Wathesalonike 3:12 Bwana na awaongeze na KUWAZIDISHA KATIKA UPENDO, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
13 apate kuifanya imara mioyo YENU IWE BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
Ni kuitendea kazi neema ya Kristo maishani mwetu. Kwa kumtii yeye, na kumfuata kwa mioyo yetu yote, nguvu zetu zote, akili zetu zote na roho zetu zote, Ambayo inafuatana pia na bidii katika kujitenga na maovu, Ndipo itakuwa rahisi sisi kuyashinda,kwasababu ataiachilia nguvu yake ya ushindi itende kazi ndani yetu, na hivyo tutajikuta tunakaa mbali na mambo ya kulaumu.
1Wathesalonike 5:22 jitengeni na ubaya wa kila namna.
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu MHIFADHIWE MWE KAMILI, BILA LAWAMA, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Hivyo ndugu uliyeokoka, tambua kuwa kila mmojawetu atatoa hesabu yake mbele za Mungu, siku ile. Hatuna budi sasa kuishi kama watu wanaotarajia TAJI bora, na sio watu wasio na mwelekeo wowote. Bwana asije akaona “neno ndani yetu”, mfano wa yale makanisa 7 tunayoyasoma katika Ufunuo 2&3, ambayo Yesu aliyapima akaona mapungufu. Hivyo tuishi kama watu wenye malengo, sio tu wa kukombolewa, bali pia wa kukamilishwa.
2Wakorintho 6:3 TUSIWE KWAZO LA NAMNA YO YOTE KATIKA JAMBO LO LOTE, ILI UTUMISHI WETU USILAUMIWE; 4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;
5 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;
6 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;
7 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
8 kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli.
Bwana akubariki.
Hivi ni baadhi ya vifungu vingine utakavyokutana na Neno hilo pia (1Timotheo 3:1-7, Luka 1:5-6)
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/03/25/kulaumu-lawama-ni-nini-kibiblia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.