Kuota unakemea mapepo/ unashindana na nguvu za giza.

by Admin | 4 July 2024 08:46 pm07

Kunaweza maanisha namna tatu, ya kwanza, ni kwamba unapitia kweli vita vya kiroho, lakini ya pili ni unaonyeshwa na Mungu uhalisia wa vita vya kiroho, na tatu unaonyeshwa uwezo wa hali yako ya  kiroho.

Maandiko yanasema

Waefeso 6:12  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama

Tukianza na maana ya kwanza,

Mara nyingine adui huanzisha mashambulizi kuanzia ndotoni, wakati mwingine utakuta mtu anaota ameumwa labda na nyoka kidoleni halafu  anapoamka, anashangaa kinauma kweli, na kama haiishii hapo, anaanza kuona kidole kinazidi kutengeneza kidonda, mpaka kuleta madhara mwili mzima, sasa hayo ni mashambulizi ya kipepo. Na hivyo ikiwa ndoto yoyote umeiota ambayo unaona uhalisia wake mpaka nje, unashindana na mapepo halafu linakukaba, unahangaika kitandani. Ujue ni mashambulizi ya adui, hapo unayo mamlaka ya kubatilisha, kwa jina la Yesu.

Lakini mara nyingine, utajikuta unaota tu unakemea mapepo, unashindana nayo. Si kwamba utakuwa unamashambulizi ya adui, lakini unaonyeshwa tu uhalisia wa vita vya kiroho, na hivyo vipo halisi, au vitakuja mbeleni katika safari yako ya maisha, na unapaswa uvishinde, kwa jina la YESU, kwa simama imara ndani yake..

Na mwisho ni Mungu anakuonyesha kiwango cha kiroho, ulichopo au unachopaswa uwe nacho. Mwingine atakuwa ameokoka, lakini anahofu ya kutoa pepo au kuombea watu, Mungu anakuonyesha uwezo wa kushindana na nguvu za giza unao, au unapaswa uanze kazi ya kuwaombea wengine wanaosumbuliwa na nguvu za giza. Lakini pia pale unapojiona umezidiwa nguvu zao, ni kuonyesha uongeze kiwango chako cha kiroho, kwa maombi, utakatifu, na Neno, ili uwe thabiti rohoni kuzipinga hila za adui.

Kwahiyo kwa vyoyote vile kuona unakemea mapepo, au unashindana na wachawi kwa jina la Yesu. Ni kuonyesha kuwa ni wakati wa kusimama  imara na Bwana. Kwasababu shetani ni adui wako, na adui za ndugu zako, na hivyo unapaswa umpinge sikuzote kwa kuwa thabiti rohoni kwa wewe ambaye umeokoka.

Lakini Ikiwa hujaokoka, basi ni vema ukafanya hivyo leo kwa kumkaribisha Yesu moyoni mwako, ukifahamu kuwa kamwe huwezi kumshinda adui kwa nguvu zako unamwita Kristo.

Ikiwa upo tayari  waweza kufungua hapa kwa mwongozo wa sala ya kuupokea wokovu. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?(Opens in a new browser tab)

Je Mungu anaketi katika giza? (1Wafalme 8:12)

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/04/kuota-unakemea-mapepo-unashindana-na-nguvu-za-giza/