by Admin | 8 July 2024 08:46 am07
Je ni kweli kuna watu wenye nyota ya bahati? Na je nitaipate nyota hiyo maishani mwangu?
JIBU: Nyota ya bahati inasadikika ni pale mtu anapobahatika kupata kitu kwa haraka au kwa wepesi, au bila matarajio yake,au nguvu zake nyingi katika kukipata tofauti na wengine. Kwamfano labda mtu ni mchimba madini, mara ghafla anatapa dhahabu nyingi tofauti na wachimbaji wengine. Au mwingine amehitimu chuo, mara anapata kazi nzuri, yenye cheo, zaidi hata ya wengine wengi waliomtangulia. Au ni mfanya-biashara mara anapata tenda kubwa ambayo inainua biashara yake kwa kasi zaidi ya wengine. N.k.
Sasa mtu kama huyu wengi husema ana nyota ya bahati. Lakini je ni kweli?
Ukweli ni kwamba twaweza kusema ana-bahati –tu, lakini hana nyota-ya-bahati. Kwavipi.
Kwasababu mafanikio hayo, yanaweza kuondoka tena kwake, na kama yakibaki, bado bahati hiyo hainunui tunu za rohoni. Mfano amani, upendo, utu wema, imani, adili, unyenyekevu, na uzima baada ya kifo. N.k., Ni mafanikio ambayo hata mashetani huyatoa.
Lakini ni lazima ujue nyota halisi ya bahati ni ipi? Ambayo katika hiyo unaweza kupata vyote, Kisha uifuate.
Hiyo si nyingine zaidi ya YESU KRISTO. Vitabu vitakatifu vinasema hivyo, Vilevile Watu wote wanalijua hilo, ikiwemo wachawi wote, wanajimu wote, malaika wote, na mashetani yote.
Soma hapa;
Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, MAMAJUSI WA MASHARIKI walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana TULIIONA NYOTA YAKE MASHARIKI, nasi tumekuja kumsujudia.
3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
7 Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
8 Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
10 NAO WALIPOIONA ILE NYOTA, WALIFURAHI FURAHA KUBWA MNO.
11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
Ikiwa Yesu yupo moyoni mwako. Ikiwa umemwamini, kisha ukamfanya Bwana na kiongozi wa maisha yako. Jambo la kwanza analolifanya ndani yako ni kuondoa laana yote ya dhambi, ambayo humfanya mwanadamu aende kuzimu, ambayo kila mwanadamu anayo. Na wakati huo huo huyo mtu anaitwa mbarikiwa, anaitwa mtakatifu, makosa yake yote yanakuwa yamefutwa, hahesabiwi dhambi tena.
Na moja kwa moja anapewa, Roho Mtakatifu. Sasa Kazi ya huyu Roho Mtakatifu, ni kumtengeneza roho yake,kumsafisha kutoka katika ubaya kumweka katika wema, na kumfanya aweze kushinda dhambi na maovu yote.
Ndio hapo kama alikuwa mlevi, kiu hiyo inaondolewa, alikuwa mzinzi, hamu ya mambo hayo yanakufa ndani yake, alikuwa ana uchungu, furaha inaanza kujengeka, alikuwa ni mwenye hasira, upendo wa ki-Mungu unaumbika sana moyoni mwake, anaanza kupenda watu wote.
Na zaidi sana, anapokea uzima wa milele, hata akifa ghafla, haendi kuzimu, hapotei, bali anakuwa amelala tu, anasubiri siku ya ufufuo, aamshwe aende mbinguni.
Pamoja na hilo, hata yale mengine ambayo alikuwa anayatafuta au anayapata kwa shida, Yesu anampa mafanikio pia kiwepesi kwasababu aliahidi hivyo. Zile bahati ambazo anatamani azipate, Yesu anamletea mara mia (100), katika maisha yake.
Mathayo 19:28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
29 NA KILA MTU ALIYEACHA NYUMBA, AU NDUGU WA KIUME AU WA KIKE, AU BABA, AU MAMA, AU WATOTO, AU MASHAMBA, KWA AJILI YA JINA LANGU, ATAPOKEA MARA MIA, NA KUURITHI UZIMA WA MILELE.
Umeona, mwisho wa siku unakuwa umepata vyote, kwasababu kwa Yesu vipo vyote.
Huoni kuwa hiyo ni NYOTA nzuri sana ya bahati? Kwanini uende wa waganga wa kienyeji, kutafuta laana, huko? Kwasababu wale wanakurushia mapepo, ambayo mafanikio yao ni batili, ni kitanzi, mwisho wa siku ni kukuangamiza, sasa unakuwa umepata faida gani? Wakati mafanikio ya Yesu Kristo, hutajirisha wala hayana huzuni ndani yake, biblia inasema hivyo;
Mithali 10:22 Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo
Ungoja nini usimpokee Yesu leo? Ikiwa umedhamiria kwa dhati kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa namna ya kuokoka leo >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
NYOTA YA ASUBUHI.(Opens in a new browser tab)
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/08/nyota-ya-bahati-yangu-ni-ipi/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.