Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

Falaki ni nini katika biblia?

Jibu: Turejee,

Isaya 47:12 “Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 

13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na WASIMAME HAO WAJUAO FALAKI, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata”.

“Falaki” ni “elimu ya nyota na sayari na jua”.

Wanaofanya Falaki, wanaamini kuwa  “mpangilio wa nyota, mwezi na jua na sayari angani, unaathiri tabia ya nchi na tabia ya mtu/watu”. Jambo ambalo kwa sehemu moja ni kweli na sehemu nyingine uongo!.

Ni kweli Mpangilio wa Jua na mwezi, unaweza kuathiri tabia ya nchi, kama  vile vipindi vya mvua, kiangazi, au kipupwe….ipo miezi ambayo mvua inanyesha, na miezi ambayo mvua hainyeshi, ipo miezi ya kiangazi na miezi ya kipupwe…Majira ya mwezi wa 6 na 7 ni Kipindi ambacho jua linakuwa mbali na dunia na kweli nchi inaathirika na baridi kali, katika ukanda wa kusini wa dunia.

Vile vile tabia za mimea zinaathiriwa na majira na nyakati, yanayotokana na mpangilio wa mwezi na jua angani, mfano tabia za miembe kuzaa maembe zinaathiriwa na mwezi wa 12, kwamba yanapofika majira ya mwezi huo wa 12 mpaka wa 1 basi miti yote ya miembe inazaa sana, tofauti na kipindi kingine chote (kwahiyo kwa sehemu ni kweli).

Sasa kwa mantiki hiyo wana-falaki wanaamini kuwa kama mpangilio wa jua, mwezi na nyota angani unaweza kuathiri mazingira na hali ya hewa, basi vile vile mpangilio huo huo unaweza kuathiri tabia za watu, na hisia zao, na maamuzi yao na hata hatima yao!.

Kwamba kila tarehe na mwezi unabeba matukio yake kulingana na mtu na mtu, na pia kulingana na tarehe aliyozaliwa, vile vile mpangilio wa nyota na mwezi unaweza kuelezea ni kitu gani mtu atafanya, au atakitenda, au kitampata, vile vile ni bahati gani ipo mbele yake au hatari gani inamkabili.

Kwahiyo wote waliohitaji kujua mambo yatakayowapata mbeleni waliwatafuta hawa wana-Falaki, au kwa lugha nyingine wanajimu kujua hatima zao.

Lakini swali ni je! Elimu hii ina ukweli wowote na je wakristo ni sahihi kuitafuta, ili kujua hatima zetu kupitia falaki?

Jibu ni LA! Elimu hii haina ukweli wowote, mpangilio wa sayari na nyota, na mwezi hauwezi kuelezea tabia, hisia, maamuzi au hatima ya Mwanadamu!…mpangilio huo unaweza kufaa katika utabiri wa hali ya hewa na misimu ya kupanda na kuvuna (tena kwa sehemu ndogo) lakini hauwezi kutabiri maisha ya mtu.

Maisha ya mtu hayatabiriwi wala kusomwa kwa kutazama jua, au mwezi au nyota au sayari, kama ndivyo kulikuwa hakuna haja ya Kristo kuja, au hata kama angekuja basi angetuhubiria sana hiyo elimu, bali maisha ya mtu yanatabiriwa kwa KULITAZAMA NENO LA MUNGU peke yake!.

Ukitaka kujua kesho yako itakuwaje, isome biblia, itakuambia sio tu kesho utakuwa wapi, bali MILELE UTAKUWA WAPI!!!.

Utauliza vipi wale Mamajusi, mbona walioiona nyota ya Bwana YESU kutoka mashariki?.

Mungu alipenda kutumia ishara ya nyota kuelekeza utukufu wa mwanae alipozaliwa, lakini hakuwa anahubiri elimu ya nyota pale!, ni sawa na alivyotumia ishara ya Nguzo ya wingu au nguzo ya moto juu ya wana wa Israeli walipokuwa jangwani,.. ilikuwa ni kwa lengo la kuelekeza utukufu wa wana wake mahali walipo, lakini hakuwa anahubiri elimu za mawingu na moto, kwamba zikasomwe kwa bidii ili kuelezea utukufu juu ya mtu/watu.

Vile vile leo hii shetani anapenyeza elimu hii ya Nyota(Falaki) ndani ya kanisa kwa kasi sana!. Elimu hii inatoka kwa waganga na inahamia kanisani kwa kasi sana..Watu hawasomi tena biblia wanatafuta kusomewa nyota zao! Hawaombi tena kulingana na Neno wanaombea nyota kwa kurejea elimu ya falaki.

Ndugu usidanganyike!..Elimu ya nyota (Falaki) ni elimu ya shetani asilimia mia.

Kama unataka kusafisha hatima yako itii biblia, wala usitafute maombi ya kutakasiwa nyota!, hiyo ni elimu nyingine!… Vile vile ukitaka kujua kesho yako itakuwaje kasome biblia, usitafute utabiri wa kusomewa nyota kutoka kwa yoyote yule iwe mganga au anayejiita mtumishi wa Mungu.. Biblia pekee ndiyo itakayokuonyesha tabia yako na kukupa utabiri sahihi wa maisha yako ya kesho na ya milele.

Je umemwamini Yesu?, je umebatizwa ubatizo sahihi? Je umepokea Roho Mtakatifu?.

Bwana Yesu anarudi.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MSHIKE SANA ELIMU.

NYOTA ZIPOTEAZO.

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.

MIEZI 13 YA KIYAHUDI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments