Haki ni Nini katika biblia. Haki ya Mungu ni ipi?

Haki ni Nini katika biblia. Haki ya Mungu ni ipi?

Haki maana yake ni kitu ambacho mtu anastahili kukipata. Kwamfano kuishi ni haki ya Kila mwanadamu, Hakuna mtu anayepaswa kumzuia mwingine kuishi, kisa ni mwanamke au ni mfupi, au ni kichaa, au mlemavu. Maadamu tu amekuwa mwanadamu tayari anayo haki ya kuishi.

Mfano mwingine wa haki, ni mtu aliyesoma  ukahitimu katika shahada Fulani labda tuseme ya utatibu, mtu kama huyo tunasema ana haki ya kuitwa daktari kwasababu amesomea jambo Hilo.

Vivyo hivyo katika Roho. Mungu naye anayo haki yake, katika kutoa vitu vyake.

Mwanzoni ilikuwa Ili kumkaribia Mungu na kupata kibali kwake na mema yote na baraka zote ilikupasa kwanza uishike Sheria yake yote. Hivyo yoyote aliyeweza kufanya hivyo alipatiwa haki hiyo. Soma Kumbukumbu 28

Lakini Kwa bahati mbaya hakukuwa na mtu aliyestahili kumkaribia Mungu kwasababu Hakuna mwanadamu aliyekwenda katika maagizo yote ya Mungu Kwa ukamilifu wote, bila kosa. Kwahiyo tangu zamani hakukuwa na mwanadamu hata mmoja aliyefanikiwa kumkaribia Mungu. Wote walitenda dhambi (Zaburi 14:3)

Hivyo Mungu akabuni mpango mwingine wa kumwokoa mwanadamu ili awe amestahili kupokea mambo yote ya rohoni ya Mungu, ikiwemo uzima wa milele na kumkaribia yeye.

Ndipo akamleta Yesu duniani, Ili Kila amwaminiye asipotee Bali apokee kuhesabiwa haki bure, bila kutegemea Tena matendo ya Sheria. Kwasababu Kwa matendo ya Sheria hakukuonekana aliyestahili.

Hivyo Mimi na wewe tunapomwamini Kristo kama ndiye Bwana na mwokozi pekee wa maisha yetu na kuukubali msamaha wake wa dhambi, basi tunahesabiwa tumestahili kuitwa watakatifu, na hivyo tunamkaribia Mungu katika ukamilifu wote, kumwomba yeye na kupokea vyote kutoka kwake bila sharti. Haleluya!

Warumi 3:21-24

[21]Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; 

[22]ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 

[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 

[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 

Hivyo ikiwa umekombolewa na Yesu Kristo, basi unapaswa uwe na ujasiri wote kumkaribia Mungu, bila kutegemea ukamilifu wako,Bali Kristo tu, na hivyo utapokea mema, yote kutoka Kwa Mungu.

Waebrania 4:16

[16]Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. 

Hiyo Ndio inaitwa “HAKI itokayo Kwa Mungu” ambayo tunaipata kwa kupitia Yesu Kristo tu peke yake.

Kwa Yesu tunapokea uzima wa milele bure. Kwa Yesu Tunapokea majibu ya mahitaji yetu yote bure. Kwa Yesu tunaitwa watakatifu.

Lakini Swali ni je! Umemwamini Kristo? Kumbuka kamwe huwezi kumpendeza Mungu Kwa matendo yako pekee, Kila mwanadamu chini ya jua anamuhitaji Kristo.

Ikiwa Bado hajaokoka basi mlango upo wazi Leo. Tubu mgeukie Bwana akuponye. Ikiwa upo tayari kupokea msamaha wa dhambi Leo, na kufanywa kiumbe kipya, basi fungua hapa Kwa Mwongozo huo. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine

TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

SI KWA MATENDO BALI NEEMA.

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments