Matangamano ni nini? (Isaya 13:10)

by Admin | 23 July 2024 08:46 pm07

Jibu: Turejee…

Isaya 13:10 “Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze

 “Matangamano” ni “Mkusanyiko wa nyota” unaoonekana na kutengeneza umbile Fulani. Wanajimu baadhi wameyataja matangamano hayo kwa maumbile ya wanyama mbali mbali, kwamfano lipo kundi moja wamelitaja kuwa na umbile kama la N’ge, lingine kama Dubu, lingine kama Simba, lingine mapacha n.k

Kwamfano kundi la nyota lenye umbile kama la Ng’e jinsi linavyoonekana mbinguni kwa macho ya damu na nyama ni kama linavyoonekana kwenye picha hapo juu.. Lakini kwa jinsi lilivyounganishwa na wanajibu mpaka kuleta umbo kama la Ng’e ni kama inavyoonekana hapa chini..

Matangamano ni nini?

Na makundi haya ya nyota, sasa yanatumika kwa unajibu (ambayo ni elimu ya shetani asilimia mia) kwaajili ya utambuzi wa majira na nyakati za watu, Elimu hii kwa jina lingine inaitwa FALAKI, Fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

Elimu hii wanajimu wanaitumia kutabiri mambo yajayo juu ya mtu, ndio hapo mtu anaenda kusomewa nyota yake na kufanyiwa utabiri, jambo ambalo kiuhalisia ni elimu ya giza, mtu yule anakuwa haambiwi mambo yajayo bali anapangiwa mambo yajayo na ibilisi, akidhani ndio katabiriwa.

Sasa Elimu hizi za Falaki pamoja na ibada zote za jua na mwezi na sayari, Bwana Mungu kazilaani, na siku za mwisho Jua, na mwezi vitatiwa giza, na Nyota zote za mbinguni zitaanguka na Matangamano yote yatazima.. kuonyesha kuwa mambo hayo yaliyotukuka kwa wanadamu si kitu mbele za Mungu, na Bwana atawaadhibu waovu pamoja na ulimwengu, ndivyo maandiko yasemavyo.

Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.

Kuhusiana na unabii wa kufutwa kwa Mwezi, nyota na sayari zote siku za mwisho pitia maandiko haya Yoeli 3:15, Marko 13:24,  Mathayo 24:29, na Ufunuo 6:12.

Kwahiyo ndugu usiende kusoma gazeti kwa lengo la kutafuta utabiri wa nyota, ni machukizo kwa Bwana, usiende kwa waganga ili wakakusafishie nyota, kinyume chake ndio unaenda kuharibu maisha yako, badala yake mfuate Bwana YESU naye atayasafisha maisha yako.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MKUU WA GIZA.

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?

MKUU WA GIZA.

Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?

AGIZO LA UTUME.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/23/matangamano-ni-nini-isaya-1310/