by Admin | 7 September 2024 08:46 am09
Jibu: Turejee..
Wakolosai 4:6 “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea MUNYU, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.
“Munyu” ni kiswahili kingine cha “chumvi”. Neno hili limeonekana mara moja tu katika biblia..
Hivyo hapo maandiko hayo yanaweza kusomeka hivi…
“Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea CHUMVI, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.
Sasa swali; Maneno yaliyokolea Munyu/chumvi ndio maneno gani?.
Kabla ya kuyaangalia haya maneno hebu tujifunze matumizi ya chumvi.
Mbali na kwamba chumvi ni kiungo cha kuongeza ladha ya chakula, lakini pia ilitumika kwaajili ya kuhifadhia vitu ili visiharibike.
Enzi za zamani hakukuwa na friji kama tulizo nazo sasa, hivyo kitu pekee kilichotumika kuhifadhia chakula ambacho hakijapikwa ilikuwa ni chumvi?.
Kwahiyo chakula kilichotiwa chumvi kilidumu muda mrefu, na kitu kingine chochote..
Soma zaidi kuhusu Agano la chumvi hapa》》Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)
Sasa tukirudi katika “maneno” ni hivyo hivyo… “maneno yaliyokolea chumvi/munyu” mbali na kwamba ni maneno yaliyokolea ladha za kiroho..Lakini pia ni “maneno yenye kidumu muda mrefu”…yasiyopita!
Ni maneno yenye kidumu si mengine zaidi ya yale yenye kutangaza habari za uzima wa milele.
Ni maneno yenye kutangaza tumaini lililopo ndani ya YESU..maneno yenye kumpa mtu hamasa ya kumtumikia Mungu ili awe na nafasi katika ule mji mtakatifu..
Ni maneno yote yaliyonenwa na YESU mwenyewe…
Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
Lakini maneno yasiyo na munyu ni yale yote yenye kunia na kutukuza mambo ya duniani ambayo yapo leo na kesho hayapo..
Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.
Bwana atusaidie maneno yetu yakolee munyu daima.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)
Ninyi ni chumvi ya dunia, Andiko hilo lina maana gani?
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/09/07/munyu-ni-nini-wakolosai46/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.