Maana ya Mathayo 6:34 ‘Yatosha kwa siku maovu yake’ 

by Admin | 11 September 2024 08:46 pm09

SWALI: Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema.. “Yatosha kwa siku maovu yake”.

Mathayo 6:34

[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.


JIBU: Bwana, hataki tuwe na hofu ya vitu vya huko mbeleni (ambavyo bado havijafikiwa), si mpango wa Mungu tubebe mizigo mingi kwa wakati mmoja, kwasababu hatujaumbiwa asili hiyo, ndio maana hata katika ile sala ya Bwana tunasema; utupe “siku kwa siku” rikizi yetu.

Hasemi utupe riziki ya “mwaka mzima” kana kwamba tukikosa vyote leo hatutaishi.. bali siku kwa siku..

Kwanini iwe hivyo?

Sasa katika hali yetu ya kibinadamu tunajua kabisa mihangaiko yetu, taabu zetu, shughuli zetu za kila siku, mara nyingi huwa haziwi safi kama tunavyotarajia, wakati mwingine kama sio kujikwaa, basi tunakutana na mambo mengi pia ya kukosesha yasiyompendeza Mungu. Hayo ndio maovu yake.

Tunakutana na watukanaji, na wazinzi, na waharibifu, wenye mizaha, wasumbufu, n.k. hivyo kiuhalisia katika mambo yetu mema, maovu pia hutokea. Hivyo kitendo cha kuyataabikia sana ya mbeleni, tafsiri yake ni kuwa tunayaleta na maovu yake pia leo. Na matokeo yake tutalemewa na maovu kichwani Na kujikuta tunamkosea Mungu.

Bwana anataka tupambane kwanza na yale ya leo, ya kesho tutapewa nguvu ya kushindana nayo. Kwa tafsiri nyingine ikiwa wewe ni wa kubeba mambo mengi ya mbeleni, dhambi itakulemea na kukushinda.

Yatosha kwa siku maovu yake.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?

Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!

HAMJAFAHAMU BADO?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/09/11/maana-ya-mathayo-634-yatosha-kwa-siku-maovu-yake/