by Admin | 7 November 2024 08:46 am11
Swali: Neno la Mungu linasema Katika Yohana 3:18 na 36 ..amwaminiye mwana anao uzima wa milele, asiyemwamini hana uzima? .. Je kuna haja ya kutafuta jambo lingine tena baada ya kumwamini Bwana YESU?.
Jibu: Yapo maandiko katika biblia yanayokamilishwa na maandiko mengine, yako maandiko ambayo hayahitaji kukamilishwa na mengine kwani yanakuwa yamejitosheleza lakini yapo ambayo yanaelezwa kwa ufupi hivyo ni lazima yakamilishwe na maandiko mengine…
kwamfano andiko hilo la Yohana 3:18 na 36 ni kweli maandiko yanatuonyesha kuwa “tukimwamini Bwana YESU hatutahukumiwa bali tutapata uzima wa milele”.
Yohana 3:18 “AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu…..
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Lakini tukirejea Marko 16:16 tunaona kuna jambo lingine linaongezeka..
Marko 16:16 “Aaminiye na KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa”.
Hapa kinachoongezeka ni “UBATIZO” Kwamba mtu akiamini pasipo kubatizwa bado hataurithi uzima wa milele, (ikiwa amesikia habari za ubatizo na hajataka kubatizwa).
Na ubatizo unaozungumziwa hapo sio ule wa MAJI TU, bali hata ule wa ROHO MTAKATIFU soma Luka 3:16.
Ili tuzidi kuelewe vizuri lugha hii, hebu tafakari kauli hizi mbili… “Ukipanda maharage utavuna maharage”… na kauli ya pili “Ukipanda maharage na kuyamwagilia maji utavuna maharage”.. Je kwa ni kauli ipi ipo sahihi kuliko nyingine?.. Ni wazi kuwa kauli zote zipo sahihi, isipokuwa ya pili imefafanua vizuri.. na inayofaa Zaidi ni hiyo ya pili, kwasababu ndio imekamilisha kauli ya kwanza.
Vivyo hivyo Neno linasema katika Yohana 3:18 kuwa amwaminiye YESU hatahukumiwa, lakini Marko 16:16, inakamilisha vizuri Zaidi kwamba Amwaminiye YESU na kubatizwa hatahukumiwa..Kwahiyo ya pili ni ya nzito Zaidi kwasababu imeikamilisha ile ya kwanza.
Sasa kwanini Imani pekee yake haitoshi ni lazima kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu??
Jibu: Kwasababu hata Mashetani yanaamini lakini bado hayana wokovu..
Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda VEMA MASHETANI NAO WAAMINI NA KUTETEMEKA.
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai”
Kwa hitimisho ni kwamba “IMANI YA KUMWAMINI BWANA YEESU ni LAZIMA IENDE NA MATENDO”.. Na tendo la kwanza ni hatua ya ubatizo wa Maji na nyingine ni ya Roho Mtakatifu.
Mtu anapomwamini Bwana YESU na kubatizwa kwa maji na kwa Roho anakuwa amekamilika, na kukidhi vigezo vya kuuona ufalme wa Mungu, kwani maana pia ya kuzaliwa mara ya pili ni kuzaliwa kwa maji na kwa ROHO.
Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU.
6 KILICHOZALIWA KWA MWILI NI MWILI; NA KILICHOZALIWA KWA ROHO NI ROHO.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?
TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;
Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/07/je-kumwamini-bwana-yesu-pekee-inatosha/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.