Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;

by Admin | 23 December 2024 08:46 am12

SWALI: Biblia humaanisha nini kwenye vifungu hivi?

Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.


JIBU: Ni vema kwanza kufahamu kwanini watu wanapigana vita?

Zipo sababu nyingi,baadhi ya hizo ni hizi,

Kujilinda, kutoelewana, kulipiza visasi, kutofautiana kiitikadi, au kutanua ngome.

Hivyo ili watu kufikia malengo hayo, njia pekee waionayo ni kutumia silaha, kuuana. Lakini biblia inashauri njia iliyo bora zaidi ambayo inaweza kutumiwa na hatimaye yote hayo yakatatulika. Na njia hiyo ni hekima.

Hekima ni nini?

Hekima ni uwezo wa kipekee utokao kwa Mungu, unaomsaidia mtu kuweza kupambanua, au kutatua, au kuamua jambo Fulani vema. Hivyo kupitia hekima mtu anaweza kuponya vitu vingi pasipo uharibifu wowote, na kuunda mfumo bora.

Sulemani ambaye ndiye aliyeyaandika maneno hayo alijaliwa amani katika ufalme wake, sio kwamba hakuwa na maadui wanaomzunguka hapana, bali alipewa hekima ya kuishi nao, na kuzungumza nao, na kukubaliana nao, hivyo Israeli hakukuwa na kumwagika damu kama ilivyokuwa kwa baba yake Daudi, ambaye yeye kutwa kuchwa alikuwa vitani. Kilichoweza kumsaidia ni hekima ya Mungu ndani yake.

Lakini sehemu ya pili ya mstari huo anasema;

Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi’.  Akiwa na maana mkosaji mmoja (wa hekima), jinsi anavyoweza kuharibu mipango mingi mizuri ambayo huwenda ilikuwa tayari imeshaleta matokeo mema. Na kweli hili angalia mahali penye viongozi wabovu, huathiri jamii nzima, hata Israeli, Wafalme wa kule ndio waliisababishia Israeli kunajisika kwa muda mrefu hadi kupelekea kwenda utumwani Babeli mfano wa hao walikuwa ni Yeroboamu na Ahabu.

Kwa ufupi vifungu hivi vinatueleza uzuri wa hekima, lakini pia madhara yasababishwayo pale hekima inapokosekana, hata kwa udogo tu.

Je! Mtu anawezaje kupata hekima?

Hekima chanzo chake ni kumcha Mungu. (Mithali 9:10). Ambapo panaanzia kwenye wokovu, kisha kuendelea kuishi maisha ya utii kwa Kristo baada ya hapo.

Mtu wa namna hii, huvikwa, ujuzi huo wa ki-Mungu, na hivyo anakuwa na uwezo wa  kuutibu ulimwengu kwa namna zote. Mioyo, Ndoa,kanisa, jamii, taifa, vyote huponywa kwa hekima msingi huu wa hekima ya ki-Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.

Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/23/mhubiri-918-hekima-ndiyo-bora-kupita-silaha-za-vita/