ANZA MAPAMBANO MWANZO WA MWAKA MPYA.

by Admin | 28 December 2024 08:46 am12

Jina la Mwokozi Mkuu, YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia.

Kosa moja maarufu Mfalme Daudi alilolifanya katika maisha yake, (ingawa baadaye alikuja kusamehewa na Bwana), lilikuwa ni kumuua Uria na kumchukua Mke wake aliyeitwa Bathsheba.

Lakini tukifuatilia chanzo cha kosa, tunaona lilianzia katika MWANZO WA MWAKA MPYA, wakati ambao Wafalme wanatoka kwenda vitani, ila yeye Daudi hakutoka kwenda vitani pamoja na wenzake badala yake akakaa nyumbani, na matokeo yake ni shetani kupata nafasi ya kumjaribu.

2Samweli 11:1 “Hata ikawa, MWANZO WA MWAKA MPYA, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. LAKINI DAUDI MWENYEWE AKAKAA YERUSALEMU.

2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?

4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.

5 Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito”.

Laiti Mfalme Daudi angalisimama na kwenda vitani pamoja na wenzake, asingeingia kwenye jaribu kubwa kama lile, ambalo liliuharibu mwaka wake wote na kumchafulia heshima yake kwa vizazi vyote.

Yote hayo ni makosa aliyoyafanya MWANZO WA MWAKA, kumbe kuna kitu katika Mwanzo wa Mwaka, vile vile na katika Mwisho wa Mwaka,..Mwanzo wa Mwaka ni wakati wa kuanza mapambano, si wakati wakulala tena, ni wakati wa kukusanya nguvu ya pamoja na kuingia katika mapambano, ni wakati wa kukusanyika katika nyumba ya MUNGU kupambana kiroho na kuangusha ngome, ni wakati wa kuomba sana.

Bwana atusaidie tuwe na mipango mema katika mwanzo wa Mwaka.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/28/anza-mapambano-mwanzo-wa-mwaka-mpya/