Fahamu maana ya Mithali 27:19 Kama uso katika maji ndivyo mtu na mwenzake

by Admin | 1 February 2025 08:46 pm02

Mithali 27:19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.


JIBU: Anaanza kwa kutoa mfano halisi, ili kueleza vema jambo la kitabia. Anasema kama vile maji yanavyoweza kuwa kioo kiakisicho, vivyo hivyo mioyo ya watu walio pamoja.

Kama tunavyojua ukiyatazama maji, utauona uso wako vilevile kama ulivyoyatazama, wala hayawezi kudanganya, ukiyaangalia umekunja sura, utaonekana hivyo hivyo, ukiyaangalia umevaa kofia, utajiona hivyo hivyo.

Ndivyo Mungu anavyowaona watu wawili waliojiungamanisha katika kitu kimmoja,(urafiki),  tabia ya mmoja itamwakisi mwingine, mwisho wa siku watafanana tu na kuwa na mwenendo sawa. Akiwa mmoja ni mwizi, Yule mwingine atakuwa kama yeye tu, akiwa mmoja ni mwamini mwombaji Yule mwenzake atakuwa naye mwombaji, akiwa ni mkarimu, mwenzake naye atakuwa hivyo hivyo.

Ndio sababu biblia inasema wawili hawawezi kukaa pamoja isipokuwa wamepatana (Amosi 3:3). Hivyo vifungu hivi vinatukumbusha umuhimu wa kuchagua watu sahihi wa kuambatana nao, imesisitiza tusifungwe nira ya watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwasababu kwa njia hiyo watatuambukiza tabia zao.

Hata katika kuoa/kuolewa, ikiwa umeokoka, tafuta wa kufanana na wewe, au mbadilishe kwanza awe kama wewe ndio umwoe/uolewe naye vinginevyo, unajiandaa kugeuzwa tabia kama ilivyokuwa kwa Sulemani kuoa wake wa kimataifa.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.

Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.

Amali, na kila kazi ya ustadi, inatokana na mtu kupingana na mwenzake.

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/02/01/mithali-2719-kama-uso-katika-maji-ndivyo-mtu-na-mwenzake/