by Admin | 21 April 2025 08:46 pm04
Ilikuwa ni desturi ya wayahudi kuyapa majina, maeneo yote ambayo walikutana na Mungu kipekee.
Kwamfano Yakobo alipokutana na Mungu mahali fulani palipoitwa Luzu, kwa kuona maono yale ya ngazi kushuka kutoka mbinguni, na malaika wanashuka na kukwea, hakuondoka hivi hivi bali alipaita mahali pale Betheli yaani ‘ nyumba ya Mungu’ (Mwanzo 28:10-22).
Sehemu nyingine Mungu alipowasaidia Israeli kuwapiga wafilisti kwa kishindo kikubwa, Samweli alilisimamisha jiwe na kuliita Eneb-ezeri akimaanisha ‘hata sasa Bwana ametusaidia’ na 1Samweli 7:12.
Hivyo pia tukisoma kisa cha Mfalme Sauli na Daudi, tunaona mara nyingi Daudi alipowindwa ili auawe alifanikiwa kumtoroka Sauli, lakini upo wakati ambao alihusuriwa pande zote, Daudi akawa hana namna isipokuwa kungojea tu kuuliwa palepale pangoni, sasa wakati ambapo Sauli amemkaribia sana Daudi. Taarifa za ghafla zilimfikia na kuambiwa kwamba wafilisti wamevamia Israeli, hivyo ikambidi aache kumfuatilia Daudi arudi Israeli kupambana na adui zake.
Sasa tendo hilo la wokovu halikumwacha Daudi awe vilevile kinyume chake, alipaita mahali pale Selahamalekothi
1 Samweli 23:26-28
[26]Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana kwenda zake kwa hofu ya Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake wakamzunguka Daudi na watu wake ili kuwakamata.
[27]Lakini akaja mjumbe kwa Sauli, kusema, Njoo upesi, kwa kuwa Wafilisti wameishambulia nchi.
[28]Basi Sauli akarudi kutoka kumwinda Daudi, akaenda kinyume cha Wafilisti; kwa hiyo wakapaita mahali pale, Selahamalekothi.
Selahamalekothi ni neno la kiebrania lenye maana ya MWAMBA WA KUTOROKEA.
Daudi na watu wake walipaita mahali pale hivyo kufuatana ba jinsi Mungu alivyowaepusha na mkono wa Sauli, kwa njia isiyodhaniwa/ kutegemewa hata kidogo.
Ni Ili kuendelea kukumbuka matendo makuu Mungu aliyowatendea wasizisahau wafidhili zake kabisa.
Je na sisi ni alama gani tunaacha mahali ambapo tunamwona Mungu ametutendea makuu. PENDA kuandika shuhuda zako, ili wakati ujao zikusaidie kukumbuka fadhili za Mungu umshukuru.
Kikawaida Mungu huwa anatufanyia maajabu mengi Sana kila siku, lakini tunakuwa wepesi kuyasahu, ni vema tujifunze kwa namna yoyote kutunza kumbukumbu, hata kama si kwa kuandika lakini kwa njia zozote zile, mfano wa mababa zetu hawa.
Mungu akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/04/21/nini-maana-ya-selahamalekothi/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.