Mapokeo ni nini?

by Devis | 16 July 2025 08:46 pm07

Mapokeo ni mafundisho, mifumo au taratibu zisizokuwepo ndani ya Biblia zilizotengenezwa na watu na kurithishwa kutoka kizazi hata kizazi.

Yapo mapokeo yaliyo mema na yaliyo hatari kwa Imani.. Mfano ya mapokeo mazuri yasiyo na madhara katika imani kama endapo yakifanyika kwa ufunuo ni pokeo ya kuadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu.. katika Biblia hakuna agizo la kuadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana, hivyo mtu asiyeadhimisha hafanyi makosa, lakini pia anayeadhimisha kwa ufunuo wa kutafakari ufufuko wake, pia hakosei, hivyo huu ni mfano wa pokeo lisilo la hatari.

Na mfano wa mapokeo ambayo ni hatari na yapo kinyume kabisa na Biblia, ni yale yanayofanyika ndani ya  ukatoliki, kama kuadhimisha Ekaristi pamoja na ibada za watakatifu (Hizo hazipo kabisa ndani  ya Biblia), na ni hatari kiroho, kwani kuabudu sanamu au kuitumikia Biblia imekataza jambo hilo katika Kutoka 20:4-5.

Pia mfano wa pokeo lingine lililo baya na hatari kiroho ni ubatizo wa watoto.. Pokeo hili ni maarufu sana lakini ni hatari sana, Kwasababu kwenye Biblia hamna mahali popote watoto wadogo walibatizwa, bali tunaona tu waliwekewa mikono na Bwana Yesu.

Sumu ya mapokeo mabaya  ni ile Bwana Yesu aliyoionyesha katika Marko 7:7-13, kuhusu “Heshima kwa mzazi”

Marko 7:7 “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,

8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika MAPOKEO YA WANADAMU.

9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.

10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe.

11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;

12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye;

13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa MAPOKEO YENU mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo”.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba tunaweza kuishi bila mapokeo na bado tukamwona Mungu na ni vizuri zaidi kuishi bila mapokeo kwani mapokeo mengi yanawafanya watu kuwa mateka wa elimu za uongo, ndivyo Biblia inavyosema..

Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! taratibu za kufunga ndoa yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?

TOFAUTI KATI MAASKOFU, MASHEMASI, WAZEE WA KANISA NI IPI?

KAMA MKRISTO NI LAZIMA UWE NA DESTURI HII.

Je ni Wokovu gani Simeoni aliouona? (Luka 2:30)

Matasa ni nini? (1Nyakati 28:17)

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/07/16/mapokeo-ni-nini/