JIBU: Kufunga ndoa ni agizo la Mungu, lakini Harusi ni karamu/sherehe ya Ndoa mpya. Na hizo ni desturi tu ambazo zipo katika mataifa mbalimbali kulingana na chimbuko lao. Hata taifa la Israeli walikuwa na desturi za harusi ukisoma
Yohana 2:1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.2.2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
Hivyo ikiwa ndoa mpya itaambatana na harusi kwa Mungu hakuna dhambi, wala hakuna maagizo yoyote kwenye biblia kwamba mtu akioa au akiolewa ni lazima afanyiwe harusi au asifanyiwe…Ni jinsi mtu mwenyewe atakavyopenda isipokuwa tu, tumeagizwa lolote tufanyalo kwa Neno au kwa tendo tufanye kwa jina la Yesu Kristo. Ikiwa na maana kuwa hiyo arusi isivuke vigezo vya kikristo.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
NDOA NA TALAKA:
BIBLIA INAKATAZA KUAPA, LAKINI KATIKA VIFUNGO VYA NDOA?
JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?
NINI TOFAUTI KATI YA UZINZI NA UASHERATI?
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?.
Rudi Nyumbani:
Print this post