by Nuru ya Upendo | 13 September 2025 08:46 am09
SWALI: nini maana ya Yohana 17:20
[20]Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
Ni akina nani hao ambao wataamini Kwasababu ya Neno lao, Bwana Yesu aliotaka kuwaombea?
JIBU: Sura hiyo ya 17 ni sura iliyoelezea kwa kina dua ambayo Bwana Yesu aliifanya kwa mitume wake kwa Baba.
Ambapo aliwaombea mambo kadha wa kadha ikiwemo walindwe katika umoja wa Roho, walindwe na yule mwovu, watakaswe na ile kweli.. Lakini pia Bwana Yesu hakuishia kuwaombea wao tu, bali na wengine ambao mitume wake watawahubiria injili na kuamini baadaye. Na hao pia maombi yake yalikuwa ni yaleyale kwao.
Maana yake ni kuwa watu wote walioamini kwa injili ya mitume walishiriki dua hiyo ya Kristo, Na hao si wengine zaidi ya wale watakatifu wa kanisa la kwanza, hadi sisi tuliopo sasa, hadi na wale watakaokuja baadaye.. sisi wote ni washirika wa dua ile (Yohana 17), kwasababu tumeamini katika injili moja ya mitume..
Ndio sababu kwanini maandiko yanasema Kristo anatuombea…maana yake ni kuwa sasa anatuombea kwa yule Roho Mtakatifu auguaye ndani yetu, lakini pia analituombea alipokuwa duniani ambapo sala hiyo tunaona matokeo yake hata sasa.
Waebrania 7:25
[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Hii ni kututhibitishia Kuwa pale tunapomwamini Kristo upo ulinzi usioelezeka unawekwa juu yetu, kiasi kwamba malango ya adui hayawezi Kushinda..kinachohitajika ni kutii tu.
Warumi 8:34
[34]Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Je na wewe ni mshirika wa sala hiyo ya Bwana? Kwa kumpokea Bwana Yesu? Kama ni la! Basi nafasi ni sasa mwamini Yesu upokee uzima wa milele.
Lakini pia Bwana anatufundisha namna sahihi ya kuomba..hatupaswi tu kuyaombea yale matunda tunaoyaona..bali hata na yale yatakayokuja baadaye..wale watakaokoka baadaye kwasababu ya Neno letu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
WOSIA WA BWANA YESU KWA WANAFUNZI WAKE.
MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
“Akaiona imefagiwa na kupambwa” Maana yake nini (Luka 11:26).
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/09/13/na-wale-watakaoniamini-kwa-sababu-ya-neno-lao/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.