WOSIA WA BWANA YESU KWA WANAFUNZI WAKE.

WOSIA WA BWANA YESU KWA WANAFUNZI WAKE.

Hakuna asiyejua kuwa Mzazi mwenye hekima anapokaribia kumaliza siku zake, huwa anawaita wanawe kuwapa wosia mfupi wa maisha pamoja na kuwabariki. Na Mzazi mwenye upendo ni yule anayewaambia wanawe au wajukuu wake ukweli wa maisha, na anayewapa tahadhari na anayewapa faraja na tumaini.. Na zaidi sana anapokaribia kumaliza siku zake huwa anawaambia wanawe siri ambazo walikuwa hawazijui.

Ndivyo alivyofanya pia Bwana wetu Yesu Kristo, kabla ya kuondoka kwake..Aliwaita wanafunzi wake na kuwapa wosia na kuwaonya mambo watakayokutana nayo baada ya yeye kuondoka. Alitumia masaa kadhaa kuzungumza nao mambo kadha wa kadha.

Na wosia wake huo umegawanyika katika vipengele vitano:

KİPENGELE CHA KWANZA: Ambacho ndiyo ile sura ya 13 yote, utaona Bwana anawaonya wanafunzi wake juu ya unyenyekevu, utaona anawafundisha kwa vitendo namna ya kunyenyekeana, (kwa kuonyesha kielelezo yeye mwenyewe, kwa kuchukua maji na kuosha miguu yao) na akawaambia atakayetaka kuwa mkubwa kuliko wote sharti awe mdogo kuliko wote. Na kama yeye wanayemwita Bwana ameshika miguu yao wao, inawapasaje wao?..Hawana budi kunyenyekeana sana na kujishusha baada ya Bwana kuondoka.

KİPENGELE CHA PİLİ: Ambacho ni sura ya 14 yote utaona Bwana anawapa faraja wanafunzi wake, kwamba wasiogope wala wasifadhaike atakapowaacha…kwani anakwenda kuwaandalia makao. Na anawaambia hatawaacha yatima, bali atawaletea msaidizi ambaye ndiye Roho Mtakatifu, na furaha yao itarudia tena. Nao watajiona kama vile hawajaachwa.

KİPENGELE CHA TATU: Ambacho ni ile sura ya 15 yote, Utaona Bwana anawaonya na kuwakumbusha kuwa wazae matunda baada ya kuondoka kwake, na kuwakumbusha kupendana..

KİPENGELE CHA NNE: Ambacho ndiyo ile sura ya 16 yote, Utaona Bwana anawaonya kuhusu mambo yatakayokwenda kuwatokea baada ya yeye kuondoka, akawaambia, dhiki watakazopitia na mateso, lakini wasiogope kwasababu yeye atakuwa pamoja nao.

Yohana 16: 1  “Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.

2  Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.

3  Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

4  Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi”.

KİPENGELE CHA TANO NA CHA MWİSHO: Ambacho ndiyo ile sura ya 17, ni kipengele cha Yesu mwenyewe kuhitimisha kwa kuwaombea wanafunzi wake.

Sasa hata baba anapotoa wosia kwa wanawe kabla ya kufariki kwake, Mwishoni huwa anapowaombea baraka na heri,  hawezi kuwaombea watu wa mtaani, au watu wa kazini kwake, ni lazima atawaombea na kuwabariki wale aliowausia pamoja na watoto wao, kwasababu ndio urithi wake.

Ndicho Bwana alichokifanya hapa, katika kipengele hichi baada ya kuwaambia mambo yatakayowatokea na majukumu yao, baada ya kuondoka kwake ndipo anawaombea..

Na anawaombea nini?

Jibu tunalipata mbele kidogo..(Zingatia  hivyo vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa)

Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

11  Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, KWA JİNA LAKO ULİLONİPA UWALİNDE HAWA, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

12  Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

13  Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

14  Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

15  Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; BALİ UWALİNDE NA YULE MWOVU.

16  Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17  UWATAKASE KWA İLE KWELİ; NENO LAKO NDİYO KWELİ.

18  Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.

19  Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

20  WALA Sİ HAO TU NİNAOWAOMBEA; LAKİNİ NA WALE WATAKAONİAMİNİ KWA SABABU YA NENO LAO.

21  WOTE WAWE NA UMOJA; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

22  Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

23  Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

24  BABA, HAO ULİONİPA NATAKA WAWE PAMOJA NAMİ PO POTE NİLİPO, WAPATE NA KUUTAZAMA UTUKUFU WANGU ULİONİPA; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.

25  Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

26  Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao”

Wosia huu unatuhusu sisi pia, kama tumefanyika kuwa wanafunzi wa Kristo hatuna budi kupendana, kunyenyekeana, kuwa na umoja na kuifanya kazi yake. Tukizingatia huo wosia basi tutafanikiwa sana katika huu ulimwengu.

Vile vile maombi hayo si ya mitume peke yao..bali ni ya kwetu pia.. kwasababu hapo kwenye mstari wa 20 anasema “WALA Sİ HAO TU NİNAOWAOMBEA; LAKİNİ NA WALE WATAKAONİAMİNİ KWA SABABU YA NENO LAO.”

Bwana alishatuombea miaka 2000 iliyopita na ameshatubariki na kutupa utukufu..Ni haki yetu kudai utukufu wetu na baraka zetu, na hatuzidai kwa maneno, bali kwa kuyafanya mapenzi yake, tunapofanya mapenzi yake katika ulimwengu wa roho ni haki yetu kupata baraka na heri na afya.

Bwana atubariki tuzidi kuwa na umoja na kupendana na kunyenyekeana…Na zaidi sana tuifanye kazi yake..Na mwisho tuzipokee baraka zake alizotubariki miaka 2,000 iliyopita.

Maran tha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

DANIELI: Mlango wa 10

MWAMUZI WA KWELI:

MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.

KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA.

UMUHIMU WA KUOMBA MSAMAHA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Eunice Tengwa
Eunice Tengwa
1 year ago

Nashukuru Sana Kwa mafundisho yenu

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen amen mtumishi. Ubarikiwe Sana.