“Akaiona imefagiwa na kupambwa” Maana yake nini (Luka 11:26).

“Akaiona imefagiwa na kupambwa” Maana yake nini (Luka 11:26).

Swali: Bwana YESU alisema pepo anapomtoka mtu na baadaye akirudi na kukuta nyumba yake imefagiliwa na kupambwa huenda kuchukua pepo wengine saba,.. maaa yake nini kusafishwa na kupambwa?.. je mapepo wanapenda sehemu safi?


Jibu: Awali ya yote tuisome mistari hiyo.

Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,

25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.

26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.

Sasa kabla ya kujua nini maana ya “kufagia na kupambwa” hebu tuelewe kwanza maana ya nyumba kiroho..

Maandiko yanasema Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu..

1 Wakorintho 6.19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Soma pia 1Wakorintho 3:16 utaona jambo hilo hilo..

Sasa kama miili yetu imekusudiwa iwe Hekalu/nyumba ya Roho Mtakatifu, maana yake ni kwamba isipokaliwa na Roho Mtakatifu basi itakaliwa na roho chafu za mapepo, maana yake badala ya mwili kuwa Nyumba ya Roho Mtakatifu, sasa inakuwa ni nyumba ya mapepo.

Hivyo mpaka hapo tumeshaelewa kuwa Nyumba inayozungumziwa hapo katika Luka 11:25-26, si nyingine zaidi ya miili yetu.

Sasa swali la pili: Nini maana ya kupambwa na kufagiliwa.

Hebu tena tutumie maandiko tujue mapambo ya nyumba ya Mungu (yaani miili yetu) ni yapi, na mapambo ya mapepo ni yapi.

1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.

Angalia mstari wa tatu (3) anasema.. Kujipamba kwenu KUSIWE!, Zingatia hilo neno KUSIWE!!.. Maana yake ni kwamba mapambo yake ni kwamba mapambo yafuatayo si ya ki Mungu bali ni ya Ibilisi, ndio maana anasema hapo KUSIWE!.. Sasa hebu tuendelee tuangalie hayo mapambo..

…”Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI..”

Oo kumbe! kuweka wigi, kuvalia mavazi (ya kikahaba), na kuvaa dhahabu masikioni na shingoni na vikuku miguuni na mikononi ni mapambo ya mapepo, na tena tumeshaona kuwa “nyumba” tafsiri yake kiroho ni “miili yetu”, hivyo tunapoweka hereni masikioni, wigi kichwani, cheni shingoni na vikuku miguuni, tafsiri yake ni kwamba nyumba zetu (yaani miili yetu) tumeipambwa kwa mapambo ya kipepo, ambayo yale mapepo yakiona yanafurahi na kwenda kutafuta pepo wengine saba, na kurudi kumwingia mtu.. Hii ni ajabu sana!.

Na ndio maana wengi (wanaume na wanawake) wanaopamba miili yao na kuvaa kikahaba wanakuwa wanasumbuliwa na mapepo na ndoto mbaya!, kwanini?..kwasababu miili yao ni nyumba iliyofagiliwa na kupambwa..

Sasa utauliza kufagiliwa ni kufanya nini?…Kufagiliwa ni maandalizi ya mapambo!..Maandalizi yote ya kiroho na kimwili kabla ya mtu kujitia mapambo ya nje ni “kufagia”..

Lakini hebu tuangalie mapambo ya ki MUNGU ni yapi!.. Tuendelee na mistari ile..

“Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu”.

Bali anasema mapambo yetu yawe Utu wa moyoni, yaani Roho ya Upole, na utulivu (kwa ufupi utakatifu).
Je! mama, dada, au kaka ni mapambo gani unayo?..ya nje au ya ndani??.. ni kweli utaonekana wa kisasa, unayekwenda na wakati, lakini fahamu kuwa mapambo hayo ndio mapepo wanayoyaangalia.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10 atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments