Kwanini Mungu alimfunga tumbo Raheli, ilihali Yakobo alimtesekea miaka 14?

Kwanini Mungu alimfunga tumbo Raheli, ilihali Yakobo alimtesekea miaka 14?

Jibu: Hakuna kosa lolote Raheli alilolifanya, lililomfanya afungwe tumbo asizae.. Lakini tukisoma maandiko twaweza kuona sababu kama mbili zilizopelekea yeye kufungwa tumbo na MUNGU mwenyewe.

 1. KUMNYENYEKEZA RAHELI na KUMTIA NGUVU LEA.

Tunasoma kuwa Lea ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzaliwa, na Yakobo alimpenda zaidi Raheli kuliko Lea, (na jambo hilo lilikuwa wazi linaonekana) kwahiyo labda ingetokea Yakobo aliyebeba ahadi za MUNGU kumuoa Raheli, na tena akazaa naye mtoto wa ahadi, huenda jambo hilo lingemfanya Raheli kujivuna/kujigamba mbele ya Lea dada yake, na hivyo Lea angekuwa duni/mnyonge mbele ya mdogo wake, kwahiyo MUNGU akamfunga tumbo.

Mwanzo 29:28 “Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe.

29 Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake.

30 Akaingia kwa Raheli naye, AKAMPENDA RAHELI KULIKO LEA, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine

31 Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.

32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.

33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.

34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.

35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa”.

2. KUKITHAMINISHA KITAKACHOZALIWA BAADAYE.

Hii ni sababu ya pili ya Raheli kufungwa tumbo: Tunasoma ijapokuwa Raheli alifungwa tumbo muda mrefu, lakini ulifika wakati akazaa, na mwana aliyemzaa alikuwa wa tofauti na wale wengine 10 waliotangulia, kwani ndiye aliyekuwa YUSUFU, ambaye alikuja kuwa Mkuu zaidi ya ndugu zake wote, na tena Mkuu juu ya nchi yote ya Misri, baada ya Farao.

Ikifunua kuwa si kila kinachochelewa kina laana!.. Vingi vinavyochelewa ni kwasababu ya Utukufu wake, hivyo usimwone mtu kachelewa kupata mimba ukamdharau!.. Hujui atakayekuja kumzaa ni nani!..
Vile vile usihuzunike unapoona unachelewa kupata mtoto, kwani vizuri na vya thamani, vina gharama, na gharama yenyewe yaweza kuwa fedheha, matusi, kejeli na masimango.. Lakini vinavyokuja baada ya gharama hizo vinakuwa ni vizuri, endapo tu utazidi kusimama katika imani, haijalishi muda, vitatokea tu!.

Wagalatia 4:27 “Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume”.
Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.

Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)

Raheli aliwalilia vipi watoto wake?

Zeri ya Gileadi ni nini?

Tunguja ni nini katika biblia? (Mwanzo 30:14).

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments