Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)

Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)

Swali: Tukisoma Mwanzo 2:23, tunaona Mwanamke Hawa  pekee ndiye aliyetajwa kama “Nyama na mfupa wa Adamu” kwasababu alitwaliwa kutoka kwa Adamu..lakini tukiruka mpaka kwenye kitabu hicho hicho cha Mwanzo 29:14, tunaona Labani anamtaja Yakobo kama “Nyama yake na mfupa wake”. Sasa swali Yakobo atakuwaje nyama na damu ya Labani, ukilinganisha na kauli hiyo ya Adamu aliyomwambia Hawa?

Jibu: Tusome mistari hiyo..

Mwanzo 2:22 “na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, NA NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume”

Turejee tena..Mwanzo 29:12-14

Mwanzo 29:12 “Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni NDUGU WA BABAYE, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari. 

13 Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.

 14 Labani akamwambia, Ndiwe kweli MFUPA WANGU NA NYAMA YANGU. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja”. 

Kauli ya “Mfupa na Nyama”, haipo tu kufunua au kuwakilisha mahusiano ya mke na mume, bali pia mahusiano ya kindugu.

Watu waliozaliwa familia moja, hao ni watu wenye mfupa mmoja na nyama moja, hata vipimo vya kibinadamu (vya kibaolojia) vinathibitisha hilo. Sasa Hawa alitwaliwa kutoka katika ubavu wa Adamu hivyo ni lazima atakuwa tu uhusiano wa kibaolojia na Adamu, na tukirudi katika hiyo habari ya Labani na Yakobo, tunasoma walikuwa ni mtu na mjomba wake, hivyo walikuwa ni ndugu (nyama moja na damu moja na mfupa mmoja).

Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa kauli ya “nyama moja na mfupa mmoja” Haikutumika tu kwa Adamu na Hawa bali pia kwa watu wenye mahusiano ya kidamu, na inatumika mpaka leo, ni sawa tu na kauli ya Mungu aliyosema kuwa “alimwumba mtu kwa mfano wake na sura yake (Mwanzo 1:26-27)” haikumfunga kwamba itumiwe na yeye tu, kwani tunaona Adamu alipomzaa Sethi katika Mwanzo 5:3 alisema maneno yanayokaribia kufanana na hayo kuwa “alizaa mwana kwa sura yake na mfano wake”. Hivyo hata sisi ni sura na mfano wa wazazi wetu, licha tu ya kuwa na sura na mfano wa Mungu.

Na watu wote waliookoka, ni wa Damu moja na mfupa mmoja na nyama moja (mwili mmoja) na Yesu Kristo.

Wakolosai 3:15  “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa KATIKA MWILI MMOJA; tena iweni watu wa shukrani”.

Waefeso 4:4  “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

5  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja”

Na wote walio damu moja na Kristo ndio ndugu zake Kristo, na hao ndio watakaorithi pamoja naye, kwasababu agano la urithi siku zote lipo kwa watu wenye undugu wa kidamu.

Je umefanyika kuwa mrithi wa ahadi za Mungu?.. Kumbuka tunafanyika kuwa warithi kwa njia ya kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

HAPANA MFUPA WAKE UTAKAOVUNJWA.

Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

JE UMEKUFA PAMOJA NA NANI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Yes
Yes
10 months ago

Haleluya