Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

Swali: Je mapepo yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai kama mawe, milima, bahari, maji au nyumba, na hata kubadilisha maumbile ya hivyo vitu?

Jibu ni LA! Mapepo hayawezi kuviingia vitu visivyo na uhai bali yanaweza kuvitumia vitu visivyo na uhai.. mapepo hayawezi kuyaingia mawe au maji au mchanga au maji kama vile yanavyoingia ndani ya mtu, na kuviendesha vitu hivyo kama yanavyowaendesha wanadamu… Sehemu pekee ambayo mapepo yanaweza kuingia ni ndani ya viumbe hai kama wanadamu na wanyama, basi!

Biblia imerekodi mara kadhaa mapepo kuingia ndani ya watu (Luka 8:27) na pia ndani ya wanyama soma Marko 5:12-13. Lakini hakuna mahali popote panapoonyesha mapepo yamewahi kuingia ndani ya mawe au katika maji au katika mchanga, au katika matofali au katika gari la farasi au katika chakula..

Mapepo yanachoweza kufanya ni kuvitumia tu vitu vya asili, kwamfano yanaweza kuvumisha upepo lakini si kuingia ndani ya upepo, vile vile yanaweza kutetemesha ardhi lakini si kuiingia ardhi, yanaweza kuitikisa bahari lakini si kuiingia bahari… uwezo ambao hata sisi wanadamu tunao, sisi tunaweza kuvumisha upepo tukiwa na kifaa kinachoitwa feni, lakini si kuuingia upepo, vile vile tunaweza kutengeneza mawimbi ya bahari kwa vyombo maalumu n.k, lakini hiyo haimaanishi kuwa tumeiingia bahari na kuiendesha bahari kama vile tunavyoiendesha mikono yetu au miguu yetu.

Na mapepo ni hivyo hivyo, hayana uwezo wa kuviingia vitu visivyo na uhai.

Kwahiyo tunachopaswa kufanya ili roho za mapepo zisiweze kutumia vitu vya asili kutuletea matatizo ni sisi kudumu katika usafi na utakatifu pamoja na kuomba… tukifanya hivyo shetani na mapepo yake hawawezi kutumia vitu vinavyotuzunguka kutuletea madhara, hawawezi kuzitumia nyumba zetu kama vituo vyao vya mikutano.

Lakini tusipojisogeza karibu na Mungu, basi shetani atatumia vitu vyote kutudhuru, atatumia ardhi, bahari, mabonde, na magari na hata nyumba kutuletea matatizo…

Isaya 13:21 “Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.

MAJINI WAZURI WAPO?

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?

Je ni viatu gani Musa aliambiwa avivue?  Vya mwilini au vya rohoni? (Kutoka 3:5).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Stany ndume
Stany ndume
1 year ago

Habari zamda uhu,naomba kuombea kudumu katika yesu