Ndugu Msomaji, nakukaribisha katika ukurasa huu kupata maarifa ya rohoni, Awali ya yote nakutahadharisha kuwa mitandaoni kuna elimu nyingi za uongo, Hivyo uisamini kila kitu mtu anachokuambia, kwasababu wengine, hawana nia njema wapo kwa ajili ya kutangazama biashara zao, na hawana lolote la kukusaidia kiroho.
Sasa turudi katika kutazama majini, na kazi zao.
Nataka ufahamu kuwa ufalme wa Roho, upo katika pande kuu mbili tu!
Hakuna upande wa hapo katikati..
Upande wa Mungu yupo Mungu mwenyewe pamoja na malaika zake watakatifu. Na upande wa Shetani, Yupo shetani na malaika zake(Mapepo), Haya mapepo ndio wale malaika walioasi mbinguni, na kwa jina lingine wanaitwa MAJINI.
Usidanganywe na mwanadamu yeyote chini ya jua kukwambia kuwa kuna majini wazuri..Huo ni uongo mkubwa sana. Hakuna majini wazuri, majini wote ni roho za mashetani zinazofanya kazi duniani kuangamiza roho wa watu, na lengo lao kubwa ni kuwapeleka watu kuzimu..Na ndio maana nakuambia chukua tahadhari mpendwa. Mafundisho ya mashetani yalitabiriwa kutokea sana katika siku hizi za mwisho
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
Pengine ulishawahi kukutana na watu wakikueleza juu ya majini wazuri, na wabaya akakutajia mmojawapo kati ya hawa..
Haya yote ni mapepo ya kuzimu, na mbali ya kuwapeleka watu kuzimu huwa yanafanya na kazi nyingine pia za kuiharibu dunia na jamii,
Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile”.
Luka 13:11 “Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.
Luka 13:11 “Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.
12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.
Luka 11:14 “Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu”.
Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba”,
Sasa, watu wanawadanganya watu na kuambiwa , jini(Pepo) ukitaka kulituma au likikuingia, fauta taratibu Fulani za asili kulitoa, labda aidha chukua majivu changanya na hiki au na kile, au andika maneno kwenye karatasi jeupe fanya hivi au vile, au ukilala angalia juu, au chukua udongo wa makaburini uchanganye na maji ya bahari na hiki au kile…Mambo kibao, Na ukifanya hivyo basi utaweza kulitoa jini hilo, au kulituma kufanya kazi Fulani.
Ndugu kama ulishawahi kufanya hivyo, ujue kuwa hukulitoa wala hukulituma, bali ndio umelikaribisha ndani ya maisha yako kukuharibu.
Idadi ya mapepo ulimwenguni ni kubwa sana, na yapo yanazunguka zunguka duniani kila mahali (Ayubu 1:7), hivyo kwa namna moja au nyingine ikiwa hujafahamu njia ya kufanya yasikukurabie basi utateswa sana. Na wengi wanadhani mpaka yawepo ndani yako, ni mpaka yatakapojidhihirisha..Hilo jambo si kweli, Mapepo ni roho, na yanafanya kazi kwa njia nyingi, mtu anaweza kuwa ni jini ndani yake lakini lisijidhirishe hata kidogo, lakini utamjua tu huyo mtu kwa tabia ya kitofauti aliyonayo.
NIFANYE NINI ILI MAJINI YASINIFUATE?
Lakini habari njema ni kuwa, yupo mmoja tu, anayeweza kumtoa mtu Mapepo/Majini kabisa kabisa, Na NI mmoja TU anayeweza kumzuia mtu asisogelewa na hayo maroho ya mashetani ndani yake kabisa kabisa, na huyo mtu si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Ikiwa wewe ni Mkristo/muislamu, huna haja ya kuzunguka kwa waganga, au kwa watu wanaojiita mataalamu wakuondolee,au wakufukuzie mapepo katika maisha yako, hao wanakudanganya tu..unamuhitaji YESU..
Yeye pekee yake ndiye aliyeweza kuyatoa majini kama aliweza kuyatoa majini (zaidi ya 82,000) kwa wakati mmoja, kwa mtu ambaye alishindikana katika mji mzima yeye akayatoa .Na saa ile ile Yule kichaa akawa mzima..
Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini”.
Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.
31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.
32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini”.
Na wewe hivyo hivyo, ukimpokea Yesu leo katika maisha yako, atakufanya kuwa huru..Biblia inasema hivyo katika Yohana 8:36..
Je! Unataka leo Yesu akuokoe?..Kumbuka wokovu sio dini, wokovu sio fedha..Wokovu ni bure kwa watu wote watakaompokea Yesu, Hivyo, kama upo tayari leo akubadilishe, unachopaswa kwanza kufanya ni kukubali kuacha dhambi zako zote, Kisha unatubu, na baada ya hapo Yesu atayabadilisha maisha yako.
Sasa kabla sijakwenda kukuombea neema ya Yesu, ikuponye hapo hapo ulipo..Fuatisha kwanza hii sala ya Toba, kwa kumaanisha kabisa..
Hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha sema maneno haya kwa Imani,
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.
Sasa upo tayari kuombewa..
Bwana Yesu, wewe ni yeye Yule jana na leo na hata milele, uliwaponya wale, ukaniponya mimi, utamponya na huyu ndugu aliyetubu leo hii.. Nakuomba Bwana Yesu unyooshe mkono wako umguse, roho yake, uyaguse maisha yako, uuguse mwili wako. Chunguza kiungo kimoja hadi kingine, uone ni wapi, pana kasoro umponye Bwana Yesu kama ulivyomponya Yule kichaa. Nguvu zote za giza zinazomsumbua mwili wake, au familia yake, au biashara yake, au ajira yake, leo hii nazitangazia mwisho wake kwa jina lako YESU KRISTO. Natuma moto wa Roho Mtakatifu ukayafunike maisha yake kama ulivyofunika Ayubu kuanzia leo na hata milele.Asante Bwana Yesu kwa kumponya. Amen.
Bwana Yesu, wewe ni yeye Yule jana na leo na hata milele, uliwaponya wale, ukaniponya mimi, utamponya na huyu ndugu aliyetubu leo hii.. Nakuomba Bwana Yesu unyooshe mkono wako umguse, roho yake, uyaguse maisha yako, uuguse mwili wako. Chunguza kiungo kimoja hadi kingine, uone ni wapi, pana kasoro umponye Bwana Yesu kama ulivyomponya Yule kichaa. Nguvu zote za giza zinazomsumbua mwili wake, au familia yake, au biashara yake, au ajira yake, leo hii nazitangazia mwisho wake kwa jina lako YESU KRISTO. Natuma moto wa Roho Mtakatifu ukayafunike maisha yake kama ulivyofunika Ayubu kuanzia leo na hata milele.
Asante Bwana Yesu kwa kumponya. Amen.
Sasa ikiwa umefuatisha maelekezo yote, kuanzia hichi kipindi utaanza kuona jinsi Yesu atakavyotembea na wewe maishani mwako. Hivyo usiache kujifunza Neno la Mungu lililo hai. Mwisho kabisa wa somo hili kuna masomo mengine ya kiroho, anza kuyapitia ujifunze ukue kimaarifa.
Pia kama utahitaji msaada zaidi, wa kupata mafundisho ya mara kwa mara kwa njia ya email. Au whatsapp yako, na ubatizo, basi wasiliana nasi kwa namba hizi : +255789001312
Bwana akubariki sana. Na hongera kwa wokovu.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
MAJINI WAZURI WAPO?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
I have much to say bt no time I didn’t know what to do bt I which we met at WhatsApp we took more 0740862988 WhatsApp number
Jamani mm niko kenya bt mniombee juu nahangaika sana na maisha
Uko Kenya sehemu gani,Mimi Niko Malindi but sai Niko Saudi Arabia nitakusaidia kaa utafuata Sheria zangu
Mi niko saudia naomba usaidizi email yangu skalama57@gmail.com insha Allah utanitafuta
Nimekutumia ujumbe kwenye email…pia waweza wasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312
0702809304 Whatsapp
Mungu mkuu was binguni asikie maombi yako na akulinde
amen
Kila jambo lawezekana kwa mungu 2
Jini alata ni jini la aina ngani
Nataka kujuga na chama yenu wadugu zangu ila na mie natamani ni we kama yiyi
Michael
Naomba nakala hii ili niweze ku print.
Amen
Neno la pepo limitimia kwa kusema mwana wa mungu kamwaga damu!!!. Mshindwi na mlegee mkewake mungu maria wapotovu
Mniombe
Unapitia nini ndugu?
Nimekutana na jini anasoma biblia
Leave your message mrng.mimi silas mamati naomba unisaidie kwa my mamu ako naiyo shida ya majini
Tutafute kwenye namba zetu za simu YESU peke yake ndiye atakayemfungua
+255693036618
Awezaye kumlinda mtu kutokamana ni kila aina ya shari ni mungu tu ambaye hana mwana wala hana ndugu yeyote katika ulimwengu huu