by Nuru ya Upendo | 17 October 2025 08:46 pm10
Watu wengi wanatamani kuona Kristo, akiwatendea miujiza, akiwaponya, akiwabariki, lakini hawataki kufikia kiwango cha uwepo wake ambacho, anaweza kuachilia nguvu zake kukuhudumia kiharaka.
Katika biblia tunaona kuna nyakati Yesu, alikuwa anatembea kufanya huduma, na umati mkubwa ulikuwa unamfuata, lakini walioponywa haukuwa umati wote, bali watu baadhi, ambao walifanya kitu cha ziada.
Yule mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12, ambaye alihangaika kwa waganga wa kila namna, asipate, uponyaji, alipomwona Yesu, na kutazama umati mkubwa wa watu, haku “assume” (dhani), kwamba kwa kumwona tu Yesu inatosha, kwa kusikia tu sauti yake inatosha, mimi kufunguliwa na yeye..
Bali alijua ni lazima nimfikie alipo, nifanye chochote, kwa namna yoyote ikiwa nitashindwa kumkumbatia, basi nitalishika tu pindo la vazi lake Inatosha..maadamu tu, kuna mahali nimeji “connect” na yeye, Nimekaribia vya kutosha.
Ndipo akaonyesha jitihada nyingi kulivuka lile Kundi, na wale walinzi (mitume wake), waliokuwa wakimlinda Yesu. Hatimaye akafanikiwa.
Luka 8:43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
Wakristo wengi leo, wanaona uvivu kumkaribia sana Kristo, wanataka waponywe wakiwa mbali, wakiwa maofisini mwao, wamekaa kwenye viyoyozi, wanatazama mahubiri youtube, lakini muda wa Kwenda ibadani hawana, wanataka wafunguliwe kwa kuletewa mafuta ya upako yaliyoombewa makanisani, lakini wao wenyewe kukaa chini kuomba hawataki, wanataka, waponywe kwa kuombewa na watumishi, lakini wao wenyewe kuutafuta uso wa Mungu hawataki..
Ndugu, lazima uutafute uwepo wa Kristo kwa nguvu.. Mambo mengine hayatoki, hivi hivi, onyesha bidii kufikia walau pindo la vazi la Yesu, umguse.
Kumgusa Yesu, ni kuhudhuria maombi ya masafa marefu, mfano mikesha..Kumgusa Yesu, ni kuwepo kwenye ibada, mahali ambapo mwili wa Kristo umeungana wote kwa uwepo wa watakatifu wengi, kumgusa Yesu ni kumsifu na kumwabudu Mungu kwa muda wa kutosha, kufunga na kuifanya kazi yake..
Lakini tuwapo walaini laini, tunangojea Yesu aletwe na watu kama barua za posta, wakati wewe mwenyewe unaouwezo wa kumfikia, utakawia sana ndugu, kama wale makutano, utafuata sana, mpaka utachoka, ni wasaa wa kuamka na kujiunganisha na Yesu wako.. Mguse, Mguse, utapokea hitaji lako kwa haraka zaidi, kuliko kuwa mbali
Ondoa uvivu wa kiroho, anza sasa kujishughulisha kwake, na yeye atakuhudumia kwa neema zake.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MISTARI YA BIBLIA YA UPONYAJI.
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/17/ufikie-uwepo-wa-mponyaji/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.