MISTARI YA BIBLIA YA UPONYAJI.

MISTARI YA BIBLIA YA UPONYAJI.

Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate ‘Neno la siku’ kila asubuhi. Na mistari mingine mingi ya faraja ..kwa link hii >>>> https://chat.whatsapp.com/LO2BncRILtiAlnRYfZWG2V

Mistari ya biblia ya uponyaji.


Inawezekana wewe ni mgonjwa na pengine unapitia katika hali ya kukata tamaa kabisa ya kupona, au unao ugonjwa usioponyeka mfano Ukimwi au Kansa, lakini nataka nikuambie jambo moja, kwa mwanadamu ni kweli haiwezekani lakini kwa Mungu hakuna linaloshindikana,

Hapo kabla nilikuwa ninasikia tu shuhuda za watu wengine kuponywa, nikadhani pengine mimi sistahili, lakini nilipokuwa katika dhambi siku moja Yesu Kristo aliniponya ugonjwa wangu wa sikio uliokuwa unanisumbua kwa muda mrefu, Na hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa kumtazama Kristo kwa sura nyingine, na kuendelea hapo aliniponya mara kadhaa tena katika vipindi tofauti tofauti nilipougua..Kama alinifanyia mimi niliyekuwa na dhambi, atakufanyia na wewe pia.

Kwa maana Yesu mwenye upendo yeye mwenyewe alituambia hivi..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.

Hivyo nawe pia unapoitafakari mistari hii, nakuombea kwa Mungu ikafanyike Uponyaji mkubwa ndani ya mwili wako na maisha yako kwa ujumla, katika jina la YESU KRISTO.

Ifuatayo ni mistari ya biblia ya uponyaji:

Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.

Zaburi 30:2 “Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya”.

Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.

2Wafalme 20:5 “Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana”.

Zaburi 146:8 “Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki”;

3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”.

Yeremia 17:14 “Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu”.

Zaburi 118:17 “Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana”.

Zaburi 119:50 “Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, Ya kwamba ahadi yako imenihuisha”.

Mathayo 8:17 “ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu”.

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,

Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Mathayo 14:14 “Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao”.

Yeremia 30:17 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye”.

Isaya 57:18 “Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. 19 Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya”.

1Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”.

Mathayo 9:35 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”.

Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana

Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana”.

Zaburi 6:2 “Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika”.

Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.

2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika”.

2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwafuraha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu”.

Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao,

Zaburi 107:19 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao,

21 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.”.

Zaburi 103:2 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.

3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote”

Kumbukumbu 7:15 “Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao”.

Hosea 14:4 “Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha”.

na kwa kupigwa kwake mliponywa

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

*****

Amini!, Endelea kuamini, uponyaji wako hakika umekufukia.

Tafadhali Share, na kwa wengine ujumbe huu wa faraja,.

Pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya biblia kwa njia ya email au  kwa Whatsapp tutumie ujumbe kwa namba hii: +255693036618 / +255789001312

Mada Nyinginezo:

YESU MPONYAJI.

Aponywa Ukimwi.

Ameponywa kansa iliyokuwa katika hatua ya Nne.

RABI, UNAKAA WAPI?

MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

MWAMBA WENYE IMARA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
16 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Sebastian
Sebastian
7 months ago

Habari,,kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri ya kutangaza neno la Mungu. Naombea nguvu zaidi, mwenyezi akawawezeshe na kuwaongezea pale mtakapopungukiwa.

Mimi ni moja ya watu wanaotamani kumjua Mungu na kuenenda kwenye njia zake. Nilitamani kujiunga kwenye group la WhatsApp lakini naona link haifanyi kazi. Kama mnaweza kunisaidia namba yangu ya WhatsApp ni 0684 477 727

Asante, na Mungu awabariki sana. Amen.

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Nimebarikiwa nakusogezwa hatua1 mbele kwa habari yakumtumaini Mungu katika ugonjwa wowote mtu anapitia kwa kua tayari tumekwisha kuponywa utukufu ni kwa Mungu.

Felix Mshana
Felix Mshana
1 year ago

I am happy to find this page
Please ray for each other including me, nimepata BP inanisumbua sana, pia kuna kitu kimauta mguuni sielewi ni nini , napaka dawa hakiishi. Naomba mniombee sana

Jovitha Joshua
Jovitha Joshua
1 year ago

Naomba mnisaidie kumuombea mama yangu anaumwa kifua naomba Mungu amponye na magonjwa ya kifua kuanzia Sasa🙏🙏

Glory nyoni
Glory nyoni
2 years ago

Mungu akubariki sana ,nimejifunza kuusu uponyaji umeniongezea kitu kwanye akili yangu

Jiloh Isai Elkanah
Jiloh Isai Elkanah
2 years ago

Nashukuru kwa kupata ujumbe muhimu wa uponyaji na kusimulia neno hili hapo juma pili mbarikiwe.

Dominic Sumary
Dominic Sumary
3 years ago

Ni Baraka sana kushirki sala za maandiko matakatifu kuhusu uponyaji. BWANA akubariki

Naftali chaula
Naftali chaula
2 years ago
Reply to  Dominic Sumary

FRANK EDWARD
FRANK EDWARD
3 months ago
Reply to  Naftali chaula

Mungu akubariki kwa masomo mazuri