Siku ya kujiliwa inayozungumziwa katika  1Petro 1:12, ni ipi?

by Nuru ya Upendo | 20 October 2025 08:46 pm10

1Petro 1:12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

Siku ya kujiliwa ni wakati ambao, Mungu anashuka ulimwenguni, aidha kwa kuokoa au kuhukumu.

Zote mbili ni siku za kujiliwa.

Kwa mfano kwa lengo la kuokoa. Upo wakati ambao neema ya Mungu humjia mtu, au taifa, na hivyo wakati huo mara nyingi uamsho mkubwa huwa unapita, Kwamfano, kipindi cha Kristo, kilikuwa ni kipindi maalumu cha Israeli kujiliwa lakini hawakukubali ..isipokuwa wachache..(Luka 19:41-44)

Lakini kwa lengo la hukumu ni siku ambayo kila mmoja wetu atahukumiwa kulingana na matendo yake.

Hivyo tukirudi kwenye 1 Petro 1:12, inayosema ‘Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa’.

Maana yake, matendo mema ya mwamini, hupelekea watu kuupokea wokovu na kumtukuza Mungu,siku neema yao inapowafikia, kwamfano wapo watu ambapo kwa kukuangalia, kwa kipindi kirefu, siku ya kujiliwa inapowafikia inakuwa ni rahisi kuamini na kumtukuza Mungu, kwasababu walishawahi kuona watu waliokoka walivyo na sifa zao njema, mfano upendo, amani, uadilifu..Lakini ukiwa na mwenendo mbovu, siku yao ya kujiliwa inapowafikia, wakikumbuka mwenendo mbovu waliouna kwako , ni ngumu sana kumtukuza Mungu,

Ndicho ambacho mtume Petro alikuwa anakieleza hata mbeleni kidogo, kuhusiana na Wanandoa, kwa upande wa wanawake, akasema, ikiwa mtu ana mume asiyeamini, anao uwezo wa kumvuta ndani ya Kristo kwa mwenendo wake tu.. (1Petro 3:1).

Kwa ufupi ni kuwa mwenendo wako mwema hulainisha njia ya neema ya Kristo Kutenda kazi vema juu ya mtu.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.

MILANGO YA KUZIMU.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/20/siku-ya-kujiliwa-inayozungumziwa-katika-1petro-112-ni-ipi/