by Nuru ya Upendo | 24 October 2025 08:46 pm10
Ni vema kufahamu Kanisa ni nini?
Kanisa sio jengo, au mahali, bali ni watu, walioitwa Na Mungu, waliookolewa wanakusanyika pamoja katika nia moja kumwabudu na kumtumikia yeye.
Hivyo watu hawa wanaweza kukusanyika maeneo yaliyo rasmi, lakini pia maeneo yasiyo rasmi kwa shughuli zao za kiibada..maadamu tu wamekidhi vigezo hivyo vya kiroho.
Kanisa la kwanza lilikusanyika Hekaluni (mahali rasmi kwa shughuli za kiibada tu). Lakini pia lilikusanyika majumbani…wakati mwingi pembezoni Mwa mito na kwenye madarasa..
Matendo ya Mitume 2:46
[46]Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Matendo ya Mitume 5:42
[42]Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Kama tunavyojua majumbani mahali ambapo, pana shughuli nyingi wakimaliza ibada huwenda sherehe zinafanyika hapo, au vikao vya kijamii, lakini hilo halikuwazuia kutimiza makusudi ya Mungu yaliyoyakusudia.
Hivyo yaweza kuwa ni sahihi endapo, hakuna mahali rasmi bado, ibada zinaweza kufanyika kwenye majengo ya shule, kwenye mabwalo, kwenye kumbi,.viwanjani, hata chini ya miti maadamu tu umoja huo upo na nia ni Kristo..hata hivyo yapo makanisa makubwa na yamefanikiwa lakini bado hayana maeneo yao rasmi ya kukutanikia…lakini kanisa Limesimama.
Mambo tu ya kuzingatia, ni nidhani yenu, adabu na utulivu wa mazingira ya kiroho kwa wakati huo,..ikiwa haya yapo hapo Mnapokusanyikia basi Mungu yupo nanyi..wala si dhambi.
Lakini ni busara na vema zaidi kanisa likatafuta eneo rasmi la kukusanyikia litakalokuwa ni kwa shughuli zao tu za kiibada.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/24/je-ni-sahihi-kutumia-kumbi-za-kidunia-kuendeshea-ibada/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.