USIWAOGOPE WAZAMZUMI

by Nuru ya Upendo | 10 November 2025 08:46 pm11

Turejee..

Kumbukumbu 2:20 “(Nchi hiyo nayo yadhaniwa kuwa ni nchi ya Warefai, hapo kale Warefai walikaa humo; lakini Waamoni huwaita Wazamzumi;

21 nao ni watu wengi, WAKUBWA, WAREFU, KAMA WAANAKI; lakini Bwana aliwaangamiza mbele yao; wakawafuata wakakaa badala yao”

Wazamzumi walikuwa ni watu warefu na wakubwa na wenye nguvu walioishi nyakati za kale, mfano wa hao ni akina Goliathi..

Watu hawa katika enzi za kale ndio watu waliokuwa wanatisha na kuogopeka sana.. walikuwa ni hodari wa vita na wenye maendeleo makubwa,  walijenga miji mikubwa na walikuwa na silaha zenye nguvu, hakuna Taifa lililowaweza kwa uhodari wao.

Lakini pamoja na kusifika kuwa na nguvu nyingi za mwili, na uhodari mkubwa, bado mbele za MUNGU mazamzumi wote si kitu, Goliathi aliangushwa na kijana Daudi aliyekuwa mtumishi wa MUNGU, Mazamzumi waliokuwepo Yeriko waliangushwa na vijana walionekana dhaifu wa kiisraeli, na zaidi sana Mazamzumi wote waliangamizwa na Bwana wakati wa gharika ya Nuhu (Mwanzo 6:4).

Kama Zamzumi wako ni “dhambi” mwambie Bwana amwangushe..kwa nguvu zako hutaweza.. kama Zamzumi wako ni kikundi cha watu fulani wabaya.. mwambie Bwana akuondolee hao watu, haijalishi ni hodari kiasi gani au wana uwezo kiasi gani, bado MUNGU ana uwezo wa kuwaondoa.

Unachopaswa kufanya ili Mazamzumi yote yaondoke ndani yako nan je yako, ni wewe kumwamini Bwana YESU na kukubali kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na pia kutafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia maishani mwako na kukutakasa kabisa kabisa.

Ikiwa bado haujabatizwa na unahitaji msaada huo basi wasiliana nasi kwa namba zetu.

Bwana YESU akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Simoni Mkirene aliubeba msalaba wa Bwana Yesu au la?

Je! aliyemwua Goliathi ni Daudi au Elhanani.

Maana ya Mithali 29:21 “Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe”

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Konstantino mkuu ni nani, na je anaumuhimu wowote katika ukristo?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/10/usiwaogope-wazamzumi/