by Nuru ya Upendo | 23 December 2025 08:46 am12
Swali: Mtakatifu wa Israeli anayetajwa katika Isaya 30:9-12 ni nani hasa? Na anakomeshwaje?
Jibu: Turejee..
Isaya 30:9 “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;
10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.
“Mtakatifu wa Israeli” anayezungumziwa katika maandiko hayo na mengine mengi, si mwingine zaidi ya MUNGU MWENYEZI, ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI, Huyo ndiye aliye Mtakatifu ambaye alifanya Agano na Israeli, Tunalithibitisha hilo zaidi katika maandiko yafuatayo..
Sasa tukirejea hayo maandiko hapo anaposema “…MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.. kukomesha kunakozungumziwa hapo sio “kule kutoa adhabu” tunakokuelewa, bali ni kitendo cha “Kuzuia jambo lisiendelee kufanyika(kufikisha jambo kikomo)”.. Hivyo andiko hilo lilihusu watu waasi ambao hawapendi sheria za MUNGU, na hivyo wanataka kuambiwa tu maneno laini na manabii, maneno ya faraja si ya kukemewa makosa yao, na lengo la kutaka kusikia hivyo ni ili WAKOME (Yaani wasiendelee) kumwangalia MUNGU, na MUNGU pia aache kuwaangalia.
Kwahiyo Mtakatifu wa Israeli ni MUNGU MWENYEZI, na ndiye pekee anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa, na mtu anayejitenga naye ni kwa hasara yake mwenyewe.
Isaya 48: 17 “Bwana, mkombozi wako, MTAKATIFU WA ISRAELI, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata”.
Mistari mingine inayomtaja Mungu kama Mtakatifu wa Israeli ni pamoja na Isaya 12:6, Isaya 47:4, Isaya 17:7, Isaya 30:12, Isaya 47:4, Isaya 48:2 na mingine mingi..
Je umemwamini YESU?.. Fahamu ya kuwa hakuna njia nyingine yoyote ya kumfikia MUNGU isipokuwa kwa kupitia yeye.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.
HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE
HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/12/23/mtakatifu-wa-israeli-ni-nani/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.