PETE YA DHAHABU PUANI MWA NGURUWE.

by Nuru ya Upendo | 24 February 2026 08:46 am02

Nini maana ya “Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.”


Jibu: Turejee..

Mithali 11:22 “Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.”

Kabla ya kujua kwa undani maana ya mstari huu, hebu tujifunze kidogo juu ya Nguruwe, na pete inayowekwa puani mwake.

Nguruwe ni mnyama mwenye sifa ya uchafu, na asiyekuwa na ustaarabu, anaweza kuoshwa na baada tu ya kumaliza kuoshwa akarudi kwenye matope..Biblia inatuthibitishia hilo..

2Petro 2:22 “Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”

Sasa pamoja na tabia hiyo ya uchafu na kukosa ustaarabu nguruwe waliyonayo, bado wana tabia nyingine ya kuchimba chimba chini ya ardhi, au kwenye mashamba na kwenye zio kwa kutumia “pua zao” kwa lengo la kutafuta chakula, au utofauti wa mazingira.

Tabia hiyo ya kuchimba chimba kwa kutumia pua, inawafanya kubeba tabia nyingine ya uharibifu usiokuwa wa kawaida,

Sasa wafugaji wa nguruwe ili kulidhibiti hilo, huwa wanaweka pete katika pua zao lengo ni ili wanapojaribu kuchimba chimba kwa kutumia pua zao, basi ile pete iliyowekwa puani iwaumize na waache au kupunguza tabia hiyo ya uharibifu.

Sasa hizi pete si za urembo, bali zinakuwa kama Hereni kwenye pua ya nguruwe, na zinakuwa ni za chuma..tazama picha juu..

Sasa inapotokea Mfugaji anamwekea nguruwe pete ya dhahabu badala ya chuma isiyo na thamani..itakuwa ni jambo la ajabu sana na la kushangaza..kwani nguruwe kamwe hajawahi kuthamini kitu cha thamani, na hata yeye mwenyewe hajithamini soma Mathayo 7:6

Sasa anapowekewa kitu cha thamani puani mwake, ni kitu cha ajabu na kinachoshangaza..

Kwa mantiki hiyo hiyo Biblia inajaribu kuufananisha uzuri wa mwanamke na PETE YA DHAHABU, na mwanamke asiye na busara inamfananisha na NGURUWE.

Kwamba Mwanamke aliye na uzuri wa uso halafu akakosa busara ni sawa na kitu cha thamani kilichowekwa mahali pasipostahili.

Mwanamke mzuri wa uso/wa nje halafu hana heshima kimwonekano ni sawa na pete puani mwa nguruwe,

“Uzuri” na “Busara” ni lazima viende pamoja, lakini ukiwa ni mzuri halafu huna busara ya kiMungu, unafananishwa na nguruwe.

Sasa swali ni je hii busara inapatikana wapi?

Chanzo cha Busara halisi ni YESU KRISTO, kwamba unapompokea YESU na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, basi hapo tayari umeshafungua mlango wa busara kuumbika nakuanza kufanya kazi ndani yako.

Na kazi hiyo ya kujaza  busara ndani yako ni ya Roho wa Mungu atakayeingia ndani yako baada ya wewe kuokoka….Utaanza kuona  kiwango chako cha hekima kinaongezeka, na ueledi katika masuala ya kiroho na kimwili.. na hiyo busara itaulinda uzuri wako wa nje na ule wa ndani kama maandiko yanavyosema..

Mithali 2:10 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;

11 Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale nguruwe. Akawapa ruhusa.

USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.

Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.

Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?

Kwanini Mungu aliwazuia walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake?(Walawi 21:16-24)

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/02/24/pete-ya-dhahabu-puani-mwa-nguruwe/