Kwanini Mungu aliwazuia walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake?(Walawi 21:16-24)

Kwanini Mungu aliwazuia walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake?(Walawi 21:16-24)

SWALI: Kwanini katika agano la kale Mungu aliwazua walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake? Ikiwa Mungu hana upendeleo kwanini aliliagiza hili litendeke?


Mambo ya Walawi 21:16-24

[16]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

[17]Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[18]Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

[19]au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

[20]au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

[21]mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[22]Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.

[23]Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.

[24]Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

JIBU: Agano la kale lilikuwa ni taswira ya agano jipya (la rohoni) jinsi litakavyokuwa baadaye (Wakolosai  2:17).

lile lilikuwa ni agano la mwilini, hivyo mambo mengi yalipaswa yadhihirishwe kwanza ki-mwilini ili kufunua au kufundisha kwa urahisi mambo ya rohoni yatakayokuja baadaye, lakini kiuhalisia haikuwa mpango wa Mungu mkamilifu yachukiliwe vilevile kwa majira yote.

Kwamfano mtoto mdogo anapoanza kujifunza hesabu, huwezi kumwambia  moja jumlisha na tatu ni nne. hatakuelewa. Bali utachukua kitu chenye umbo, (labda vijiti). utampa kimoja, kisha utachukua tena vijiti vingine vitatu utampa. halafu utamwambia avichanganye avihesabu atoe jumla.  atavihesabu vyote..na hapo hapo anakuambia nimepata vinne.

Sasa yeye atadhani hesabu ni vijiti. Lakini anapokuwa mtu mzima anagundua alipewa tu maumbo ili aelewe vizuri. Lakini hesabu ni uelewa wa akilini sio vijiti.

Vivyo hivyo na sisi tulipoanza kuelezwa makusudi makamilifu ya Mungu, tulifananishwa na watoto (Wagalatia 4:1-6). Mungu hakutaka kumleta Kristo moja kwa moja afe, amwage damu yake, ndipo sisi tuondolewe dhambi zetu kwa hiyo damu. Ukweli ni kwamba tusingemwelewa Mungu, vema.

Hivyo alitanguliza agano la kale kwanza, la mwilini, la mambo ya nje. Tuelewe kitaswira jinsi ilivyo sawa na isivyo sawa. ndipo baadaye atumie mifano hiyo kueleza ya rohoni.

kwamfano walikatazwa kula nguruwe, sababu alikuwa hacheui, mnyama asiyecheua ni yule asiyeweza kurejesha chakula akakitafuna na kukimeza tena kama ng’ombe. Sasa lengo la Mungu sio kwasababu nguruwe alikuwa ana magonjwa. kiuhalisia nguruwe ni mboga nzuri tu, lakini ni kwasababu ya ile sifa, ya kutocheua, ambayo rohoni sisi tunafundishwa hatupaswi kuwa nayo. maana yake ukishindwa kutafakari, yale uliyotendewa na Mungu nyuma, au uliyofundishwa na Mungu, wewe ni sawa na kiumbe najisi, mfano wa nguruwe. kwasababu hutaweza kuwa mtu wa shukrani, hutaweza kuwa mtu wa imani. Wana wa Israeli walionyesha tabia hii, wakati wanavuka habari ya shamu. walimnung’unikia Mungu wakisema unatuua, kwasababu hawana chakula. hawakukumbuka miujiza mikubwa aliyowatendea kipindi kifupi nyuma. Lakini Daudi alipokutana na Goliati hakulia wala kuogopa alisema yule Bwana aliyeniokoa na dubu na simba ataniokoa na mfilisti huyu asiyetahiriwa. alicheua akala tena akapata nguvu ya kuendelea mbele, kumshinda adui. Hakutaka kuwa nguruwe.

sasa tukirudi pia katika mambo ya madhabahuni kufuatana na swali letu.  Kumbuka waliopewa nafasi ya kuhudumu hekaluni walikuwa ni jamii ya makuhani tu, wazao wa Lawi. Mtu mwingine yeyote hakuruhusiwa. Vilevile hata yule mlawi ikiwa ni mlemavu wa aina yoyote pia hakuruhusiwa.

Kuonyesha kuwa hawakutengwa wao tu, hata watu wa kabila nyingine, haijalishi ni manabii au wanamtumikia Mungu kiasi gani ikiwa wewe si mlawi hukuruhusiwa hata na wanawake wote, hawakuwa tofauti na vilema katika suala la kuhudumu. Kwahiyo hawakutengwa walemavu tu. Bali na makundi mengine yote.

Sasa kwanini Mungu akataze walemavu na wenye madhaifu wasihudumu. Kwasababu Mungu alikuwa.anaonyesha picha ya rohoni ni jinsi gani watumishi wake, wahudumu.wa madhabahuni wanavyopaswa wawe, kwamba wasiwe watu wenye kasoro mbele zake. Yaani wawe watu wakamilifu sio walemavu rohoni.

Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Mungu, hakuwa na Neno lolote baya na walemavu. Wala hakuwachukia.

Na ndio maana tunapokuja agano jipya tunaona vipofu, viwete, mabubu wanamjia Mungu, anawaponya. Na isitoshe Yesu alikuwa anakwenda kukaa kwao na kula nao (Marko 14:3).

Mungu hashughulika na ulemavu wa mwilini, bali ule wa rohoni. Ambao ukiwa mdhaifu huko, wewe ni najisi mbele zake. pitia somo hili ufahamu zaidi juu ya ulemavu wa rohoni upoje.

>>> UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

wapo walemavu wengi, ambao wengine Mungu mwenyewe ameruhusu wawe vile kwa ushuhuda wake, na wanamtumikia kwa namna isiyo ya kawaida na wanafanya miujiza mikubwa, wanaponya watu na kuwafungua, utauliza kwanini Mungu asiwaponye? mawazo ya Mungu si mawazo yetu, Elisha alikufa na ugonjwa wake, lakini mifupa yake ilifufua wafu.

fuatilia ushuhuda huu ukujenge…. >>> USHUHUDA WA RICKY:

Hii ni kutuonyesha kuwa,  wakati wa sasa mbele za Mungu hakuna mwanamume, au mwanamke, au mlemavu au mtumwa wote ni makuhani wake na tumestahilishwa na Yesu Kristo kuingia patakatifu pa patakatifu kwa damu yake sisi tuliomwamini….

Haleluya. Upendo wake ni wa ajabu kwetu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?

CHAKULA CHA ROHONI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments