FAHAMU JINSI YA KUPATA MAMLAKA YA DAMU WA YESU.

by Nuru ya Upendo | 26 February 2026 08:46 am02

Matumizi ya damu ya YESU hayaishii tu katika kutamka, kwamba tukiwa na haja na jambo tunatamka “Kwa Damu ya YESU” na jambo lile linatokea au linatii… hapana ni zaidi ya hapo, kwasababu hata mashetani wanamjua Bwana YESU na Damu yake.

Hivyo hayatishiki na mtu wa kawaida kulitaja jina la YESU au Damu ya YESU na huku mtu huyo hana uhalali, au mamlaka ya kutumia Jina hilo, soma kilichowatokea Wana saba wa Skewa (Matendo 19:4) unaweza kuelewa zaidi.

Sasa Mamlaka ya kutumia DAMU YA YESU, tunapataje?

Tunapata mamlaka ya kutumia DAMU YA YESU kwa kanuni moja tu!, nayo ni ile ya kuwa na UNDUGU WA DAMU NA YESU?

Utauliza mtu anaweza kuwa na undugu wa Damu na YESU na mwingine asiwe nao?..

Ndio!, hiyo inawezekana kabisa na nitakuonyesha kimaandiko…Lakini tambua jambo moja kuwa ili mtu aitwe ndugu yako ni lazima muwe na mfanano wa damu, mnaweza msifanane sura, au mwonekano lakini bado damu ikaeleza undugu mlio nao (hiyo imethibitika kisayansi na wanadamu).

Na YESU KRISTO anao ndugu zake wa damu.. sasa tunawajuaje?.. tusome maandiko yafuatayo Mathayo 12:47

Mathayo 12:47 “Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.

48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

50 Kwa maana ye yote ATAKAYEYAFANYA MAPENZI  YA BABA YANGU aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu”.

Umeona? Ndugu za YESU wana sifa gani?… hawana sifa ya usomi, au uzuri, au ukuu au umaarufu… bali ni wale wote WANAOFANYA MAPENZI YA BABA ALIYE MBINGUNI.

Kumbe ili tuwe NDUGU WA DAMU WA YESU, ni lazima TUYAJUE na KUYAFANYA MAPENZI YA BABA MBINGUNI?.

Je unayajua mapenzi ya MUNGU kwako?.. Kama huyajui je unawezaje kuwa na ujasiri wa kuitumia DAMU YAKE, na ilihali huna muunganiko wowote na hiyo DAMU?

Ni lazima uyajue mapenzi ya MUNGU, na KUYAFANYA.. ili ile damu iweze kunena mema juu yako (Waebrania 12:24).

Je wewe  ni ndugu wa YESU?… Je unayajua Mapenzi ya MUNGU kwako?.. kama bado huyajui au huna uhakika kama unayafanya mapenzi yake au la!, basi usikose sehemu inayofuata ya somo hili inayozungumzia MAPENZI YA MUNGU.

Waebrania 2:11 “Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;

12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.

13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.

14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa”.

Bwana atusaidie..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.

SAFARI YA KUUONA USO WA MUNGU.

Tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu ni ipi?

Nini tofauti ya kushuhudia na kuhubiri?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/02/26/fahamu-jinsi-ya-kupata-mamlaka-ya-damu-wa-yesu/