by Nuru ya Upendo | 8 April 2026 08:46 am04
Je unajua “Kumpenda Mungu sio Ombi bali ni Amri”?..Tofauti na inavyodhaniwa leo kuwa kumpenda Mungu ni jambo ambalo ni “Ombi”.. Kwamba tunaombwa kumpenda Mungu.. Lakini Biblia haitufundishi hivyo.
Biblia inatufundisha kuwa kumpenda Mungu ni Amri, (maana yake tunaagizwa kumpenda Bwana Mungu wetu kwa roho zetu zote) na pasipo kufanya hivyo ni makosa..
Mathayo 22:35 “Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
38 HII NDIYO AMRI ILIYO KUU, TENA NI YA KWANZA”
Ni madhara gani yanayoweza kumpata Mtu, anapoivunja hii amri na kumpenda miungu mingine?
Madhara yapo mengi ikiwemo kuukosa uzima wa milele katika siku ya mwisho, lakini katika maisha haya dhara lake kubwa kuliko yote ni LAANA!.
Mtu asiyempenda Bwana MUNGU wake, anajiletea laana juu yake, na uzao wake na vyote alivyonavyo..
1Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”.
Jifunze kumpenda Mungu kwakuwa yeye ndiye aliyekuumba.
Ukimpenda utamkaribisha YESU maishani mwako,
> Ukimpenda utaacha hizo dhambi unazozifanya (Zaburi 97:10)
> Ukimpenda utatafuta kujua kusudi lako kuja duniani ni lipi
> Ukimpenda hutaendelea na maisha ya uvuguvugu
> Ukimpenda hutafanya matambiko na mila
> Ukimpenda hutaabudu sanamu wala kudharau maagizo yake.
Ukimpenda utafanya yote yaliyoandikwa katika Biblia.
Kwa mapana kuhusiana na jinsi ya kumpenda Bwana kwa moyo wote, roho yote, nguvu zote na akili zote, fungua link hii hapa chini. >>
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
Zaburi 145:20 “Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
JE UNAO UHAKIKA BWANA YESU AKIRUDI LEO UNAKWENDA NAYE?.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/04/08/asiyempenda-bwana-na-awe-amelaaniwa/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.