NINAYEPENDEZWA NAYE

by Nuru ya Upendo | 25 April 2026 08:46 am04

Mathayo 3:16 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, NINAYEPENDEZWA NAYE”.

Nataka tuone hiyo sehemu ya mwisho ya andiko inayosema.. “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. hasemi ninayefurahiwa naye, au ninayeshangiliwa naye, au ninayetukuzwa naye, au au ninayeshabikiwa naye, au ninayeburudishwa naye, bali ametumia neno “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. Hili ni neno kubwa sana.

Ni lazima tutafute “kumpendeza Mungu” siku zote hilo ndio jambo kuu na Mungu analolihitaji kutoka kwetu…

Waefeso 5:9 “kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

10 MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA”.

Kumpendeza MUNGU maana yake ni kufanya mambo yanayoufanya moyo wa MUNGU kukufurahia na hayo si mengine zaidi ya matendo ya UTAKATIFU.

1Wathesalonike 4:2” Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

3 Maana haya NDIYO MAPENZI YA MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;

4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA;

5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Na utakatifu ni ule nje na ndani, sio tu wa ndani bali pia wa nje, maana yake jinsi unavyouweka mwili wako pia.

Warumi 12:1” Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

Epuka kuwa mshabiki wa MUNGU bali tafuta “kumpendeza Mungu”.. Mtu ambaye ni mshabiki wa Mungu ni yule anayejua sana mambo ya Mungu na sheria zake, lakini hazifanyi na pia hazipingi huyu ni mfano wa mtu ambaye ni mshabiki.

Ni yule mtu ambaye anakubali Mungu ni mwenye nguvu, ni wa upendo, ni mwenye haki na hata kumsifia mbele za watu, lakini kimaisha na mwenendo hamfuati MUNGU, bali anafuata njia yake, na ibilisi ndiye anayemtumikia. (huyu ni mshabiki)

Epuka kuwa mshabiki, bali kuwa mwana wa MUNGU ambaye UNAMPENDEZA MUNGU aliyekuumba. Kuwa mtakatifu mwilini na rohoni.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/04/25/ninayependezwa-naye/