Je! Hayo Mambo ya duniani na ya mbinguni ni yapi?

by Nuru ya Upendo | 2 May 2026 08:46 pm05

Yohana 3:12

[12]Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 

SWALI: Je! Hayo Mambo ya duniani ni yapi? Na hayo mambo ya mbinguni pia ni yapi Yesu aliyoyamaanisha?


JIBU: Ukianza kusoma tokea vifungu vya juu utaona sababu ya Bwana Yesu kusema maneno hayo, ni baada ya yule Nikedemo mkuu wa mafarisayo kumfuata usiku ili kumuuliza maswali, lakini Yesu akamjibu kwa kumwambia kuhusu habari za kuzaliwa mara ya pili, lakini jambo hilo likawa gumu sana kwa nikodemu kulipokea…akamweleza Bwana yawezekanikaje mambo hayo? …Ndipo Yesu mwishowe akayasema maneno hayo;

12]Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 

Sasa hapo hamaanishi alikuwa anafundisha mambo ya duniani, hapana…bali alikuwa anatumia mifano ya duniani kueleza yale ya rohoni ili iwe rahisi watu kuelewa..kwamfano hapo alitumia mifano ya mtu kuzaliwa, vilevile akatumia mifano ya tabia ya upepo kumfafanulia Nikodemu aelewe mtu wa rohoni naye anavyopaswa awe…mahali pengine alitumia mifano ya wakulima, wafanyabiashara, maharusi, wavuvi, wafalme. wanyama n.k.

Ilikufundisha ufalme wa Mungu ulivyo na unavyofanya kazi..

Lakini mambo ya mbinguni ni yale ambayo hayana uhalisia na maisha yetu ya duniani kabisa…mambo hayo huwezi yaeleza kwa mifano ya kidunia..Hivyo ni kuyapokea tu kwa imani.

Kwamfano jinsi gani hekima ya Mungu isipopatikana popote isipokuwa ndani ya Yesu Kristo. Na jinsi gani Mungu aliumba ulimwengu kwa kupitia Kristo, ambaye alikuja kama mwana aliye Mungu yuleyule (Yohana 1:1-4).

Mambo hayo hayakuweza kusadikika kwa hekima za kibinadamu, ndio maana yalifichwa yakaja kufunuliwa baadaye kwa Roho Mtakatifu kwa mitume kuwa ndiye Mungu mwenyewe katika mwili( 1Timotheo 3:16)

Ndio maana wayahudi na hata watu wengine leo hii wa dini wanashindwa kuelewa iweje Mungu awe na mtoto, wakati hana mshirika…halafu huyo huyo mtoto awe ndio yeye tena.

Jambo kama hili halina mifano ya kibinadamu ya kujitosheleza kuelezea, ni kuamini tu!…lakini kwa imani waziona kazi zake na kujua hakika Kristo ndiye Mungu mwenyewe bila tashwishwi…Hivyo amini tu, uelewa kamili utaufahamu ufikapo mbinguni, ni sawa na Yesu alivyomwambia Nikodemu upepo huvuna upendako, hujui utokako vilevile hujui uendako, lakini sauti yake waisikia…ndivyo ilivyo katika asili ya uungu wa Mungu.. Tunamjua Kristo kuwa ni Mungu kwa kazi zake kuu na timilifu juu ya maisha yetu.. 

Ni nini Bwana anataka wewe ujue.

Sehemu kubwa ya mambo yanayotuzunguza yanahubiri habari za ufalme wa mbinguni. Kama hatutaelewa kwa kuitafakari mifano hii, kamwe tusidhani tutaelewa yale yasiyoingia maanani kabisa tuyasikiapo.

Je! Umempa Yesu maisha yako? Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Yesu amekaribia kurudi, unasubiri nini usiokoke?

Tubu sasa upokee uzima wa milele. Ikiwa unahitaji msaada huo wa kuokoka basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;

Kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba na ushauri.

+255789001312 / +255693036618

Bwana akubariki.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?

BALI WANA WA UFALME WATATUPWA NJE!.

JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/05/02/je-hayo-mambo-ya-duniani-na-ya-mbinguni-ni-yapi/