by Nuru ya Upendo | 8 May 2026 08:46 pm05
Swali: Je ni kweli malipo ya watu wote ni hapa hapa duniani?
Jibu: Turejee Mithali 11:31, tutapata mwanga wa swali letu..
Mithali 11:31 “Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?”
Ndio madhara ya makosa yote yanaanzia hapa hapa duniani, kabla ya kufa.. Kwamfano, Neno linasema “waheshimu baba yako na mama yako upate siku nyingi na za heri za kuishi duniani (Kutoka 20:12)”.
Sasa mtu ambaye hawaheshimu wazazi wake wala kuwatii, yeye ni kuwadharau na kuwatukana, mtu huyo ataanza kulipwa hapa hapa duniani kwa kupunguziwa miaka yake ya kuishi, na sio tu miaka ya kuishi, bali pia na ya Kheri, na sio hiyo tu bali na dhambi nyingine zote, kama wizi, au uzinzi hukumu yake inaanzia hapa hapa kama mtu haQtapigwa kwa maradhi basi atapigwa kwa roho za mapepo kwani uzinzi unaunganisha nafsi za watu.
Kwahiyo utaona ni kweli, adhabu ya waovu, inaanzia hapa hapa duniani, lakini hiyo bado haimaanishi kuwa baada ya kifo hakutakuwa tena na adhabu..La! Biblia inatufundisha kuwa hata baada ya kulipwa duniani bado kuna hukumu nyingine baada ya kifo ya ziwa liwakalo moto kwa mtu mwovu.
Kwa namna gani? Tusome maandiko yafuatayo..
Ufunuo 22:8 “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo”.
Umeona?.. Kwahiyo kama mzinzi akipigwa na maradhi kutokana na uzinzi alioufanya na akafa bila kutubu, ijapokuwa kateseka duniani na maradhi, bado tena ataenda kuteseka na adhabu ya ziwa la moto, hata watu wa Sodoma na Gomora Biblia inatuonyesha kuwa watahukumiwa tena siku ya mwisho ingawa tayari walishachomwa duniani (Soma Mathayo 10:145).
Ikifunua kuwa dhambi si ya kuchezea kabisa, ina madhara hapa duniani, na kule kwenye maisha ya baada ya kifo.
Upo usemi ya kwamba, Mungu atawapunguzia adhabu wale waliokufa katika dhambi ikiwa walidhurika wakiwa duniani, nataka nikuambia, dhambi ina matokeo makubwa kote kote, huku duniani na baada ya kifo.
Tunafundishwa kuikimbia dhambi, Sasa labda unajiuliza utaikimbiaje?.. Utaikimbia kwa kuanza kujitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi na umemkosea MUNGU, baada ya hapo unachukua hatua ya kuungama, yaani kuomba toba kwa makosa yako yote, kwa kumaanisha kabisa.
Baada ya hapo, hatua inayofuata ni kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele, na Roho Mtakatifu atashuka juu yako kukutia muhuri wa milele. Kupitia Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako utaona mabadiliko ya kimaisha na kiutendaji ndani ikiwa kama hutamzimisha kwa kurudia dhambi kwa makusudi na kuacha kukusanyika na wengine.
Lakini kama utazingatia kuhudhuria vipindi vya Neno la Mungu na maombi ya pamoja, Roho Mtakatifu atakaa na wewe na hapo utakuwa umekamilisha hatua yako ya kuikimbia dhambi.
Bwana atusaidi.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU
Ipi tofauti ya Hasira na Ghadhabu ya MUNGU?.
Ni kwa namna gani YESU KRISTO atawahukumu walio hai na waliokufa?
Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/05/08/je-ni-kweli-malipo-ni-hapa-hapa-duniani/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.