by Nuru ya Upendo | 18 May 2026 08:46 pm05
Swali: Katika 1Samweli 16:7 tunasoma, MUNGU anamwambia nabii Samweli kuhusu mtu atakayempaka mafuta kama Mfalme katika nyumba ya Yese, kwamba yeye haangalii uso kama wanadamu wanavyoangalia.
Jibu: Turejee..
1Samweli 16:6 “Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.
7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, USIMTAZAME USO WAKE, WALA UREFU WA KIMO CHAKE; KWA MAANA MIMI NIMEMKATAA. BWANA HAANGALII KAMA BINADAMU AANGALIAVYO; MAANA WANADAMU HUITAZAMA SURA YA NJE, BALI BWANA HUUTAZAMA MOYO”.
Andiko hili linalenga MAUMBILE ya ASILI ya Mtu, kwamba hayo ndio MUNGU hayaangalii kama kipimo cha kumpatia mtu “haki” au “hukumu”, na mambo hayo ni kama rangi ya mtu, urefu, ufupi, ulemavu, au uzima..
Mambo hayo hayatutofautishi sisi kwa sisi mbele za MUNGU. Kwamba ukiwa mfupi au mrefu au mweupe au mweusi basi ndio unaweza kupata kibali mbele za MUNGU. La!, hayo ni mambo ambayo MUNGU hayaangalii kabisa..
Lakini jinsi tunavyoiweka miili yetu, na kuivisha na kuilisha na kuinywesha ni vitu ambavyo MUNGU anavitazama sana kwasababu vipo ndani ya uwezo wetu, lakini urefu na ufupi hakuna mtu anajipangia, ni maumbile ya asili ya MUNGU mwenyewe.
Kwahiyo mtu anapovaa mavazi ya jinsia nyingine, au yanayouchora mwili wake, hayo yanajalisha sana mbele za MUNGU (1Timotheo 2:9, Kumbukumbu 22:5), au mtu anapojichubua au kujichora mwili wake Mungu anatazama (Soma Walawi 19:28).
Kwahiyo Bwana MUNGU, aliposema Haangalii uso, maana yake hashawishwi na maumbile ya asili ya mtu. Je umempokea YESU?. Una hakika YESU akirudi leo utakwenda naye?.
Kama bado haujampokea YESU unasubiri nini? Mwamini leo na ubatizwe kwa maji na kwa Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TAFUTA UTAKASO WA SEHEMU KUU NNE ZA MWILI WAKO.
Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO.
NI NANI TUNAPASWA TUMWONE ZAIDI KILA TUSOMAPO BIBLIA?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/05/18/je-ni-kweli-mungu-haangali-utu-wa-nje-katika-kumpatia-mtu-haki-au-hukumu/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.