Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?

Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?

SWALI: Wakati shetani anamjaribu Yesu, biblia inasema alimchukua na kumpandisha kwenye kinara cha hekalu, swali ni je! Alikuwa anachukuliwaje mahali pale ni njia gani ilikuwa inatumika?


JIBU: Awali ya yote ni lazima tufahamu kuwa Bwana Yesu hakupelekwa sehemu nyingine yoyote ili kujaribiwa zaidi ya pale jangwani. Hii ikiwa na maana majaribu yake yote yalimtokea akiwa palepale jangwani.

Mathayo 4:1  “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi,2  Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa”

Sasa kama ni hivyo iweje, shetani amtoe pale na kumpeleka kwenye kinara cha Hekalu na wakati huo huo amwonyeshe milki zote za ulimwenguni? Je! Aliondokaje pale? Au alichukuliwa kimazingara?

Mathayo 4:5  “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu 6  akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7  Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8  Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9  akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. 10  Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 11  Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia”

Jibu ni kwamba majaribu yale yalikuwa katika roho, na sio katika mwili, Kwa ufupi yalikuwa ni mfano wa maono. Na kikawaida maono yanapokuja ikiwa ni ya kukuonyesha tukio husika utashangaa waweza kujiona kama upo pale pale eneo lenyewe, lakini sio. Kama tu vile ndoto. Unaota upo kijijini kwenu, anashughulika, unaongea na ndugu, lakini kiuhalisia kumbe umelala palepale kitandani.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, alikuwa palepale jangwani, wala hakutoka, isipokuwa alikuwa katika roho, akayaona hayo yote, aliyoonyeshwa na shetani.

Bwana akubariki.

Lakini pia ni vizuri, kutambua maana ya majaribu yale, Kwasababu hayo pia ndio shetani anayotumia kumjaribu kila mtakatifu aliyepo duniani. Kwa upana wa habari hiyo waweza fungua link hii >>> MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?

Tofauti kati ya ufunuo, unabii na maono ni ipi?

NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?

JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?

UFUNUO: Mlango wa 11

DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.

KWA WINGI WA WASHAURI HUJA WOKOVU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Fred
Fred
10 months ago

Ahsante kwa ufafanuzi,
Naomba kuuliza…ina maana Yesu akupelekwa kwenye ule mlima(temptation Mountain)??
Maana pale kwenye mji wa Jerico kuna uo mlima na watu uutembelea.