DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.

DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.

Hizi ni dalili 9 za mtu mwenye pepo.

1.Hofu.

Ukiona kuna hofu ndani yako isiyoisha, kila wakati unaishi katika hali ya  wasiwasi wa kitu usichokijua wala usichokiona, kila wakati unapata mshtuko na mkandamizo mkubwa wa mawazo, furaha inakuwa haidumu ndani yako, dakika yoyote unaona au unahisi kama utapoteza maisha..hizo ni roho chafu za mapepo zimekuingia, hivyo tafuta msaada wa maombezi haraka sana.

Warumi 8:15 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba”.

2. Ndoto zinazojirudia rudia.

Ukiona unaota Ndoto zinazojirudia rudia, ndani ya kipindi kifupi… na zote zina maudhui ya kishetani ikiwemo vifo, uzinzi, mauaji, au vitisho. Tafuta msaada wa maombezi.

3. Sauti.

Ikiwa unasikia sauti zinakuita jina lako au zinakupa taarifa Fulani au maagizo fulani na zinajirudia mara kwa mara, (tofauti na ukiwa katika mazingira ya kusali au katika nyumba ya ibada), Tafuta msaada wa maombezi.

4. Kiburi

Ukiona una kiburi kilichopitiliza kilichoshuhudiwa na watu wengi pamoja na chuki nyingi na vinyongo na hasira zilizopitiliza, hiyo sio hali ya kawaida…katafute msaada wa maombezi haraka sana.

5. Nguvu za Ajabu

Ukiona una nguvu za ajabu katika mwili wako, ambazo chanzo chake hukielewi katafute msaada wa maombezi.

6. Kufanya vitu pasipo kujitambua

Ukiona unafanya vitu pasipo kujitambua, (pasipo kuwa na habari)… baada ya muda kupita ndio unakuja kuambiwa kuwa ulifanya hiki au kile, au wewe mwenyewe ndio unakuja kugundua ulifanya hiko kitu pasipo kujitambua.. Katafute msaada wa maombezi.

7. Tabia chafu

Ukiona unaendeshwa na tabia chafu usiyoweza kujizuia, tafuta msaada wa maombezi.

8. Magonjwa yasiyoeleweka

Ukiona unapata ugonjwa au magonjwa yanayoonyesha tabia zisizo za kawaida, (maana yake yana badilika badilika), leo utaumwa hiki kesho kingine tofauti kabisa na cha jana, tafuta msaada wa maombezi..

9. Hamu ya kusoma Neno na kufanya Maombi

Ukiona Hamu ya kusoma Neno na kufanya maombi imepungua ndani yako kwa kiwango kikubwa, tafuta msaada wa maombezi.

Kumbuka!…Mtu mwenye pepo ndani yake kamwe hawezi kumtumikia Mungu, kwani roho hizo siku zote zinapingana na roho wa Mungu. Mtu anaweza kweli kutamani kumtumikia Mungu, lakini roho hizo zitamvunja moyo na kupingana naye na kumtesa na kumletea kukata tamaa na mateso. Hivyo ni lazima zitoke kwanza na kuwa huru ndipo aweze kumtumikia Mungu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TABIA KUU TATU ZA WAHUBIRI WALIORUDI NYUMA NA KUMWACHA MUNGU.

KWANINI MITUME WAMUULIZE BWANA FARAGHANI?

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA

EPUKA KUUNDA MATARAJIO YAKO, KWENYE AHADI ZA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NIYIKIZA
NIYIKIZA
1 year ago

NAHITAJI SOMA JUU YA ROHO ZILIZO CHINI YA MAZABAHU. AO NAMNA WALIVYOTESWA WAISRAELI

Antony Laban
Antony Laban
1 year ago

Mungu aendelee kuwainua katika kutuhabarisha Habari za mbingu Hai katika Yesu

Ezra ndambuki
Ezra ndambuki
1 year ago

Please naomba unisaindie Niko Kenya somo lako limeninguza asa 1&9 nisaindie please

Ezra ndambuki
Ezra ndambuki
1 year ago

Nikweli mwalimu wangu umenifundisha kuhusu mambo hayo na Hali sio nzuri kabisa kwa waombezi kwakua wamejichanganya na mambo ya kindunia jee nikwa njia ngani nyengine naweza tumia nikpona roho yangu kama mtumishi wangu mtiwa mafuta na MUNGU
Naweza kujiombea au ukaniombea?