ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu katika kuyatafakari maneno ya uzima.

Leo tutaona Tabia Moja ya ahadi za Mungu, na Kwa kuijua hiyo basi itakutia moyo wewe ambaye upo katika matarajio ya kuzipokea ahadi timilifu za Mungu.

Nataka tujifunze Kwa Ibrahimu. Kama tunavyojua Mungu alimwahidia kuwa atakuwa na uzao mkubwa kama nyota za mbinguni kwa idadi yake jinsi zisivyoweza kuhesabika. (Mwanzo 15:5).

Lakini katika kuzipokea haikuwa sawa na matarajio yake, Bali zilikuwa za kukwama kwama sana. Utaona Sara alikuwa mgumba, mpaka Ibrahimu anakufa aliambulia mtoto mmoja tu kutoka Kwake mwanamke aliyeitwa mama wa mataifa mengi..Lakini heri ingekuwa Kwa Ibrahimu tu, lakini bado tunaona Kwa Isaka,. Rebeka naye alikuwa na shida katika uzazi, mpaka kuwazaa wale watoto wawili yaani Esau na Yakobo, lilikuwa ni jambo la kulisumbukia sana.. Vivyo hivyo hata Kwa Yakobo, mke wake kipenzi Raheli alikutwa na matatizo hayo hayo…

Hawa wote ndio watu ambao waliahidiwa na Mungu kuwa uzao wao utaongezeka Kwa wingi Kwa mfano wa nyota za mbinguni…lakini tunaona Kila wanapotaka kuongezeka walikwama kwama.

Utajiuliza ni kwanini? 

Sio kwamba walikuwa na shida au laana za ki-ukoo kama wengi wanavyodhani..au kwasababu ya majina yao yamefungwa,  Jibu ni hapana.. kwasababu Mungu tayari alishambariki Ibrahimu kwa kumwambia atakuwa baba wa mataifa mengi, alishabarikiwa,  lakini Mungu anataka kutufundisha sisi Tabia za ahadi zake jinsi zilivyo katika baadhi ya majira.

Sasa tunaona wakati wa Mungu ilipofika  jambo hili lilikuja kugeuka ghafla. Na watu Hawa ambao walionekana ni wenye wagumba wengi.. walianza kuzaliana Kwa wingi ambao uliushtusha ulimwengu. Pindi walipoenda Misri, walianza kuzaa, Kwa kasi hata ya kulipitia taifa la Misri   ndani ya wakati mfupi sana .walienda watu sabini tu lakini Kwa muda mfupi walikaribia kulizidi taifa la mamilioni ya watu.

Ikawa tishio kubwa Kwa Wamisri, mpaka wakabuni mpango wa kuwauwa watoto wote wa kiume watakaozaliwa..lakini bado hilo halikuzuia kitu. Wakati familia Moja ya Wamisri inazaa watoto wawili, familia Moja ya kiisraeli inazaa watoto kumi na Tano. ..

Kutoka 1:8-22

[8]Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.

[9]Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

[10]Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.

[11]Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

[12]Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.

[13]Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;

[14]wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.

[15]Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;

[16]akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

[17]Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.

[18]Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?

[19]Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.

[20]Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.

[21]Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.

[22]Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.

Lakini ongezeko hilo.kubwa, halikuanza hivyo.. uhodari huo wa Waisraeli kuzaliana Kwa kasi vile haikuwa kipaji, au Hali waliyokuwa nayo tangu mwanzo, Bali walianza kama Kwa kusua-sua sana..Lakini mwisho wa siku ahadi ilipokomaa ule uwingi kama nyota za mbinguni waliuona, hakukuwa na mgumba.

Ni Nini nataka tuone?

Sikuzote jambo lolote ambalo Mungu anatuahidia, ni kawaida katika hatua za mwanzo kuenda kama Kwa kusua sua hivi, SI vyepesi kuona vikitirika Moja Kwa Moja kama wengi tunavyotarajia..Kitaanza kidogo kama unaona mwanga Fulani hivi, halafu kitasimama, baadaye Kitaanza Tena, Kisha kitasimama, kitaonyesha dalili zote za kuongezeka, Kisha hakitaendelea Tena..hivyo hivyo kinaweza pita kipindi Fulani. Sasa ukijikuta katika Mazingira kama hayo hupaswi kuvunjika Moja na kujiona kama utakuwa na makosa Fulani, au Mungu ameghahiri ahadi zake..Jibu ni hapana. Hupaswi kukata tamaa, shikilia ahadi ya Mungu, ukiamini kuwa yeye ni mwaminifu lazima atimize ahadi zake kwako, kukuongeza.

Moja siku isiyokuwa na jina. Utaona mtiririko ambao haujautarajia, itakuwa siku baada ya siku ni kuongezeka tu, Wala hakuna kupungua. Wala kukwama-kwama kama mwanzo. Lakini hiyo yote hutegemea kung’ang’ana kwako na ahadi za Mungu sasa.

Jambo hili linasimama Mahali popote pale Mungu alipoweka maono yake moyoni mwako. Iwe ni katika huduma, kazi, uzao.n.k. Usiache tu kushikilia ahadi za Mungu, Tena ufurahi kwasababu maandiko yanasema hivyo, kwani uwingi wako upo karibuni.

Isaya 54:1

[1]Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.

Shalom.

Je umeokoka? Je unamtambua kuwa Yesu yupo mlangoni kurudi? Ikiwa bado unasubiri nini? Tubu dhambi zako ukabatizwe katika jina la Bwana Yesu Kristo upokee ondoleo la dhambi zako. 

Kumbuka: UNYAKUO UPO KARIBU.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NINI NI KILICHOMFANYA IBRAHIMU AKUBALI KUMTOA MWANAWE SADAKA?

PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.

Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.

KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.

WEWE U MUNGU UONAYE.

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments